Balozi wa Oman nchini Tanzania
Mhe. Ali A. AL Mahruqi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (kushoto)
leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bi.
Debora Mkemwa.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia
Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) akizungumza jambo alipotembelewa na
Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI
anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia
Elimu Mhe. Joseph Kakunda akizungumza jambo na Balozi wa Oman hapa
nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi walipokutana leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Oman nchini Tanzania
Mhe. Ali A. AL Mahruqi akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda alipomtembelea Ofisi kwake
leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais –
TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) na Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi.
Zainabu Chaula(kushoto) wakimuonyesha Balozi wa Oman nchini Tanzania
Mhe. Ali A. AL Mahruqi kifungu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2015 kinachozungumzia utoaji wa huduma za jamii alipotembelea Ofisi za
Naibu Waziri wa huyo leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais –
TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL
Mahruqi (wa pili kutoka kulia) alipotembelea Ofisi za TAMISEMI Jijini
Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri huyo
Bi. Debora Mkemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI
anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula pamoja na mmoja wa Afisa
kutoka Mambo ya Nje ya Nchi Bw. Odiro.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
…………………….
Na Eliphace Marwa
MAELEZO
BALOZI wa Oman Ali Al Mahruqi
amesema Wafanyabiashara wa nchi hiyo wamevutiwa na na hatua mbalimbali
znazochuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga mazingira bora
kwa...
wawekezaji na wengi wao wapo mbioni kuja kuwekeza katika miradi
mikubwa ya maendeleo nchini.
Balozi Al Mahruqi aliyasema hayo
leo aJijini Dar es Salaam wa mazungumzo baina yake na Naibu Waziri Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Kakunda
na kuongeza kuwa suala la usalama wa mitaji yao ni jambo ambalo
Wafanyabiashara hao wanapenda kuhakikishiwa na Serikali ya Tanzania.
Balozi Mahruqi alisema miongoni
mwa fursa zinazowavutia Wafanyabiashara wa Oman kuja kuwekeza nchini ni
pamoja na ubora wa miundombinu katika sekta za elimu na mifugo ikiwemo
upatikanaji wa tasnia ya nyama.
“Serikali ya Oman ina mpango wa
kuja kuwekeza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kipaumbele kikubwa
kitakuwa ni nchi ya Tanzania kutokana na fursa mbalimbali za uwekezaji
zilizopo Tanzania,” alisema Balozi Mahruqi.
Aidha Balozi Mahruqi aliitaka
Serikali kuharakisha makubaliano ya mikataba baina ya Mataifa hay ili
kuwezesha wawekezaji kutoka Oman kupata fursa ya kuwekeza nchini na
kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kutoka Oman.
Kwa upande wake Naye Naibu Waziri
Kakunda alimuahidi Balozi Mahruqi kufanyia kazi changamoto zilizopo ili
kuhakikisha wawekezaji kutoka Oman wanakuja kwa wingi kuwekeza nchini
bila ya kuwa na hofu ya usalama wa mitaji yao.
“Nitafuatilia kwa kina kwa
wataalamu weu wanaohusika na uwekezaji kwenye kiwanda cha nyama ambapo
wawekezaji kutoka Oman watawekeza takribani dola milioni tatu ambazo
zitasaidia wafugaji wa Watanzania kupata soko la mifugo yao” alisema
Naibu Waziri Kakunda.
Aidha Kakunda aliahidi kufuatilia
maeneo ambayo Serikali ya Oman iliahidi kusaidia kaika ujenzi wa visima
mia moja vya maji katika maeneo ya mashule ili kupata orodha kamili ya
shule zinazotakiwa kupatiwa msaada huo.
No comments :
Post a Comment