Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaofanya
shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari , wakati wa
ziara ya kikazi aliombatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna
Makakala(watatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya mkoa huo.Lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli
mbalimbali zilizopo chini ya idara za wizara na kukagua mipaka iliyopo
katika mkoa huo
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Dkt. Anna Makakala, akizungumza na wananchi wanaofanya shughuli zao
katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati wa ziara ya kikazi ya
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa
Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam
Malima, akijibu baadhi ya hoja zilizoulizwa na wananchi wanaofanya
shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati wa ziara
ya kikazi ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (wapili kulia), akiambata na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt.
Anna Makakala (kulia)
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna
Makakala(wapili kulia),Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima() na Mkuu wa
Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga(kulia), wakisikiliza maswali ya mmoja wa
wananchi wanaofanya shughuli karibu na kituo cha Mpaka wa Tanzania na
Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua mipaka
iliyopo ndani ya mkoa huo.
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dkt. Anna
Makakala( kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima(watatu kulia)
wakisikiliza maswali ya mmoja wa wananchi wanaofanya shughuli karibu na
kituo cha Mpaka Tanzanua na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi
yenye lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani ya mkoa huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
……………..
Na Abubakari Akida-WMNN
NAIBU Waziri Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewataka wananchi na wafanyabiashara
wanaofanya shughuli zao karibu na Kituo cha Mpaka wa Sirari
unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya kuhakikisha wanashirikiana na
Jeshi la Polisi mkoani Mara kudhibiti matukio ya uhalifu kwa...
kutoa
taarifa za wahalifu hao kwa jeshi hilo.
Hayo ameyasema akiongea na
wananchi wakati wa ziara ya kikazi katika mkoa wa Mara, ikiwa na lengo
la kutembelea mipaka iliyopo katika mkoa huo inayotenganisha nchi ya
Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda ambapo katika ziara hiyo
aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Alphonce
Malibiche na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama.
“Tumekuwa tukipata taarifa
wananchi wa hapa kushirikiana na wahalifu katika kupitisha mali za
magendo hapa hasa wakitumia vijana wanaoendesha bodaboda kupitisha
mizigo yao na kuripotiwa matukio mbalimbali yanayohatarisha usalama wa
raia wetu, natoa wito kwa wananchi wa hapa kushirkiana na jeshi la
polisi kudhibiti matendo hayo ya kihalifu,” alisema Masauni
Aidha,Naibu Waziri Masauni
amewataka wananchi hao kuacha mara moja tabia inayokua kwa kasi katika
eneo hilo ya kulizuia Jeshi la Polisi kufanya shughuli zake na endapo
atabainika mtu yoyote atakumbana na mkono wa sheria huku akitoa ushauri
kwa jeshi kuzifanyia utafiti taarifa zitakazoletwa ili kuepuka kumuonea
mtu.
Akizungumza na wananchi hao
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, amewataka wananchi hao
kupeleka taarifa za wahamiaji haramu pindi watakapowagundua ili kuweza
kudhibiti tatizo la wahamiaji hao kuingia nchini huku akiweka wazi
viwango vya udhibiti vilivyoweka na idara yake kuzuia wahamiaji haramu
kuingia nchini.
“Idara ya Uhamiaji kupitia
wawakilishi wetu mkoani hapa tupo tayari na tunaomba mtu yoyote mwenye
taarifa za wahamiaji haramu azifikishe kwenye ofisi ya uhamiaji nasi
tutazifanyia kazi kwani tushapunguza tatizo hilo na tuko katika jitihada
za kulimaliza kabisa,” alisema Dk. Makakala
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taida (NIDA), Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Alphonce
Malibiche, alisema NIDA imezindua zoezi la usajili wa vitambulisho kwa
wakazi wa Mkoa wa Mara na wanatarajia kumaliza zoezi hilo mapema ili
wananchi wa Mkoa huo na wilaya zake wawe na vitambulisho vya Taifa
vitakavyozuia baadhi ya changamoto lakini lengo kubwa ni kuhakikisha
kila Mtanzania anakua na Kitambulisho cha Taifa.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments :
Post a Comment