Thursday, November 30, 2017

TANZANIA NA CHINA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA SHERIA


NA 01
Naibu Waziri wa Sheria Jamhuri ya Watu wa China Zhao Dacheng akiwasili ofisi za Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kukutana na Waziri wa Katiba na Sheria  Profesa Palamagamba Kabudi kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya sheria baina ya nchi mbili.
NA 02
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na mgeni wake Naibu Waziri wa Sheria wa China Zhao Dacheng walipokutana kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya sheria.
NA 03
Naibu Waziri wa Sheria wa China Zhai Dacheng akisaini kitabu cha wageni
NA 04
Ujumbe wa Tanzania ukioongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi ukiwa katika majadiliano na ule wa China ulioongozwa na Naibu Waziri wa Sheria Zhao Dacheng
NA 05
Wzairi wa Katiba na Sheria Profesa Kabudi akizungumza wakati wa kikao baina ya ujumbe wa Tanzania na China
NA 06
Ujumbe wa Tanzania na China ukiwa katika mazungumzo
NA 07
Ujumbe wa China katika mazungumzo
NA 08
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Mahusiano ya Kimataifa  katika Wizara ya Sheria ya China Yu Kang akizungumza wakati wa kikao baina ya Tanzania na China
NA 09
Ujumbe wa China katika majadiliano
NA 10
Waziri wa katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akipokea zawadi kutoka kwa mgeni wake Naibu Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Dacheng.
NA 11
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju  akipewa zawadi na Naibu Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Watu wa China Zhao Dacheng
NA 12
Ujumbe wa Tanzania na China ukiwa katika picha ya pamoja
NA 13
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju akizungumza na Msaidizi wa Waziri wa Katiba na Sheria Charles Mmbando  mara baada ya kumalizika kikao cha majadiliano baina ya ujumbe wa Tanzania na China
PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA-TUMESHERIA

No comments :

Post a Comment