Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
WATANZANIA
wametakiwa kuzitumia fursa zilizopo kwenye sekta ya utalii ili kukuza
kuongeza vipato na uchumi badala ya kuendelea kulalamika hali ngumu ya
maisha.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira amesema wakati wa hafla ya
...
kuwasindikiza mabalozi 9 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali
ulimwenguni wakiwemo na maafisa wa Bodi ya Utalii na Wizara ya Mambo ya
Nje wakati wakipanda mlima Kilimanjaro mkoani hapa jana.
“Hatuna
sababu ya kulalamika uchumi, utalii pekee laiti tungeutangaza vizuri
tutafika mbali. Sisi Watanzania hatuoni uzuri tulionao ukienda nchi
nyingine ndio utaona, nashauri watu wengi zaidi wapande mlima huu
tuliopewa bure na Mungu ili kuona uzuri uliokuwepo,” alisema Bi.
Mghwira.
Akizungumza
na mabalozi hao aliwashauri wakati mwingine wakifanya shughuli kubwa
kama hiyo waje nchini na raia katika mataifa wanayowakisha ili kuongeza
tija ya kujitangaza kimataifa.
“Leo
wanapanda mabalozi wachache, lakini kama wangekuja na raia mbalimbali
kutoka nchi wanazotuwakilisha tungeona zaidi ya watu 80 wanapanda mlima
huu na ujumbe ungesambaa zaidi, hivyo nashauri tutumie nafasi hizi
kujitangaza vizuri,” alisema Bi. Mghwira.
Aidha,
alishauri watu wanaoishia katikati ya safari bila kufika kileleni
wapewe vyeti kulingana na maeneo waliyofika kwa sababu kufika tu katika
mlima huo ni historia tosha si lazima kufika kileleni ndipo upewe cheti
cha utambulisho.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Bi Devota Mdachi alisema
wameandaa kazi hiyo ya mabalozi kupanda mlima kwa kushirikiana na Wizara
ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa,
TANAPA, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Bank M lengo ni kuonyesha
fursa za utalii zilizopo nchini.
“Leo
Novemba 29, 2017 mabalozi wanaanza kupanda hadi Disemba 4 ndio
tunamaliza, wakifika kileleni watatumia fursa ya kupiga picha na kuweka
kwenye mitandao ya kijamii kuitangazia dunia kuwa mlima upo Tanzania
lakini pia watahamasisha mabalozi wenzao katika mataifa waliyotoka
pamoja na wananchi,” alisema Bi. Mdachi.
Aliongeza
kuwa hiyo ni miongoni mwa njia wanayoitumia kutangaza utalii kwa sababu
mabalozi wanakutana na watu wengi pamoja na kuhamasisha raia wa nchi
wanazotoka kuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini.
Hata
hivyo, akizungumzia namna utalii wa ndani Bi. Mdachi alisema:
“Watanzania hawatembelei vivutio kwa kutofahamu kwamba kuna viinglio
vilivyo chini kwa ajili yao, TTB kazi yetu ni kuhamasisha kwa kutoa
taarifa, tumeshirikiana na mamlaka mbalmbal za utalii na sasa watalii wa
ndani wanatembelea vivutio yetu.”
Balozi
Azizi Mlima kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ambaye pia aliwahi kuwa
Balozi nchini Malaysia, alisema mwaka 2014 alishiriki kupanda mlima huo
wakiwa mabalozi 18 kwa lengo la kutangaza utalii wa mlima huo kimataifa,
ameamua kurudi tena ili kuonyesha heshima yake kwa mlima huo wenye sifa
ulimwenguni.
“Tulipopanda
mwaka 2014 kati ya mabalozi 18 tuliofika kileleni ni mabalozi 14, mwaka
huu tumerejea tena kwa lengo la kuutangaza mlima lakini pia kuhifadhi
mazingira. Tunafahamu theluji iliyo kileleni inaanza kuyeyuka na ndiyo
maana jana tulianza kwa kupanda miti ili kutunza mazingira,” alisema
Balozi Mlima.
Naye
Balozi Hemedi Mgaza anayeiwakilisha Tanzania nchini Saudi Arabia
amesema wakiwa katika balozi mbalimbali nje ya nchi huwa wanapata
maswali mengi kuhusiana na vivutio vya utalii nchini, hivyo anaamini
raia wa Saudi Arabia wakimuona amefika kileleni nao watahamasika.
Mwaka
huu wanapanda mabalozi 13 wakiwemo maafisa kutoka Bodi ya utalii na
Wizara ya mambo ya Nje kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani lakini pia
kutunza mazingira ya mlima huo, kaulimbiu ya mwaka huu ni Upandaji
Mlima Kilimanjaro Diplomasia na Utalii kufikisha katika kilele cha
Afrika.
RC MGHWIRA-TUMIENI FURSA ZA UTALII KUONDOKANA NA UMASIKINI,WATANZANIA WASHAURIWA

No comments :
Post a Comment