Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa
Mkoa wa Geita aliyevaa miwani na Koti la kijivu akimpokea Waziri wa
Madini wa Uganda Mheshimiwa Lokeris Peter baada Mkoani Geita na ujembe
wa Mawaziri wanne na wanasheria kwa ajili ya kujifunza namna Serikali
ya Tanzania inavyowawezesha wachimbaji wadogo, Kati na Wakubwa katika
Shughuli zao.
Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa
Stanslaus Nyongo Mwenye kizibao cha rangi nyukundu akiwa na viongozi wa
Mkoa wa Geita pamoja na Mawaziri wanne wa Serikali ya Uganda baada ya
Kuwasili Mkoani Geita kujifunza uchimbaji mdogo, Kati na Mkubwa wa
Madini.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi
Robert Gabriel wa kwanza kulia akiwaongoza Mawaziri kutoka Uganda kwenda
kukagua shughuli za uchimbaji mdogo Lwamgasa Wilayani Geita.
Mawaziri wanne kutoka kutoka
Uganda pamoja na viongozi wengine wa Wizara ya Madini na Mkoa wa Geita
wakujionea shughuli za ujenzi wa Kituo cha mfano cha Serikali
zinavyoendelea katika eneo la Lwangasa Wilayani Geita. Kituo hiki
kinajengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya
Dhahabu.
Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa
Stanslaus Nyongo akiongozana na Mawaziri kutoka Uganda pamoja na
wataalamu wa Madini kukagua shughuli za uchimbaji mdogo wa madini katika
mgodi wa Kadeo Lwamgasa Geita.
Mmiliki wa Mgodi wa KADEO Mine
Limited ndugu Kadeo akitoa maelezo kwa Mawaziri na wataalmu wa madini
walipotembelea Mgodi wa KADEO Mine kujifunza shughuli za uchimbaji mdogo
wa Dhahabu Kata ya Lwamgasa Geita.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa
Mkoa Geita mwenye koti la kijivu na miwani akiwaongoza Mawaziri kutoka
Uganda kukagua shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi wa KADEO.
Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa
Stanslaus Nyongo akizungumza na wadau wa madini na wanachama wa chama
cha wachimbaji wadogo wa madini katika Mgodi wa Busolwa Mine wakati wa
zaiara ya mwaziri waane kutoka Uganda ya kujifinza uchimbaji mdogo wa
Madini.
Mwaziri kutoka nchini Uganga
pamoja na wataalamu wa madini wakifuatilia kwa karibu shughuli za
uchimbaji mdogo zinavyofanyika katika Mgodi wa KADEO Limited uliopo kata
ya Lwamgasa walipokwenda kujifunza uchimbaji Mdogo.
PICHA ZOTE NA Magesa Jumapili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
……………..
Mawaziri wa nne wa Wizara za
Madini, Uchumi, Mambo ya Ndani na Nje wa Serikali ya Jamhuri ya Uganda
wamewasili Mkoani Geita kujifunza namna Serikali ya Tanzania
ilivyofanikiwa kuwezesha na kuendeleza Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu ili
kukuza Sekta hiyo nchini kwao.
Akizungumza kwa niaba ya Mawaziri
wengine baada ya kuwasili katika Mgodi wa Busolwa Mine Waziri wa Nchi na
Maendeleo ya Madini wa Uganda Mheshimiwa Lokeris Peter amesema kuwa
wamekuja Tanzania kujifunza mbinu za kuendeleza Sekta ya Madini hususan
Uchimbaji Mdogo kwa kuwa Tanzania imekuwa ikifanya shughuli hii kwa muda
mrefu na kupata mafanikio makubwa. Mheshimiwa Peter ameongeza kuwa
wamekuja Geita kwa kuwa ni kuna migodi mingi mikubwa na midogo hivyo
wamekuja kujifunza namna wanavyochimba, kuuza, kuunganisha wachimbaji
katika vikundi na namna wanavyothibiti utoroshaji wa madini ili nao
wakawaendeleze wachimbaji wa dogo nchini Uganda kwa nia ya kupata
maendeleo kama Tanzania.
Awali akizungumza katika Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Stanslaus Nyongo Naibu Waziri wa Madini amesema
kuwa Tanzania tumepata maendeleo makubwa ya kuweza kuendeleza wachimbaji
wadogo, kati na wakubwa hivyo Mawaziri wanne na Wanasheria kutoka
Uganda wamekuja nchini kuona ni jinsi gani Serikali ya Tanzania
ilivyofanikiwa kuendeleza na kusaidia uchimbaji wa madini mdogo, kati na
mkubwa. Amesema “wametembelea nchi nyingine za Afrika lakini bado
wameona kuna umuhimu wa kufika Tanzania kwasababu kila nchi waliyofika
waliona Tanzania ni mfano kwa Afrika hivyo wamekuja kujifunza na kuona
namna nchi inavyoneemesha wananchi wake kupitia sekta ya madini baada ya
mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2010 kwenda Sheria mpya ya
mwaka 2017 na mabadiliko yake na sera za nchi kwa jumla “. Ameongeza
kuwa wamekuja Geita kwasababu kuna madini na wachimbaji wadogo wengi
zaidi ili waone jinsi wachimbaji wadogo wanavyowezeshwa kupata mitaji ya
kufanya shughuli za uchimbaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza Serikali ya Uganda kwa kuona
umuhimu wa kuja kujifunza Geita na kutambua jinsi Sekta ya madini
inavyoweza kuleta mageuzi ya uchumi wa nchi. Ametoa wito kwa wachimbaji
wadogo mkoani hapa kujiunga katika vikundi ili kuunganisha nguvu, mitaji
na uzoefu wao kwa pamoja na walete vifaa vya kisasa na kuwa na
uchimbaji wa kisasa wenye tija ili mitaji yao ipanuke na kupata faida
ili kuongeza ajira nyingi kwa watanzania.
Wakiwa Mkoani Geita Mwaziri hao
pamoja na wataalamu wao wametembelea Wilaya ya Geita ambapo wamejionea
shughuli za uchimbaji mdogo na kati katika migodi ya Busolwa mine uliopo
kata ya Nyarugusu,Kadeo Mine na Kituo cha mfano cha Serikali kwa ajili
ya kufundishia masuala ya uchimbaji wa madini kilichopo eneo la Lwamgasa
Wilayani Geita.
Na: Magesa Jumapili
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
No comments :
Post a Comment