Serikali
ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert
Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita.
Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka.
Uamuzi wa
kusherehekea Siku ya Taifa ya Vijana ya Robert Gabriel Mugabe kila 21
Februari ulifanywa rasmi kupitia tangazo rasmi kwenye gazeti la
serikali.
Tangazo hilo lilichapishwa Ijumaa –
siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa aliapishwa kuwa rais, na kufikisha
kikomo uongozi wa Mugabe wa miaka 37.
Serikali ya Bw Mugabe ilikuwa
imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa sikukuu ya taifa mwezi
Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa vijana katika chama cha
Zanu-PF.
Bw Mugabe aliondolewa mamlakani
wiki iliyopita kutokana na shinikizo kutoka kwa wanajeshi waliokuwa
wamechukua udhibiti wa serikali wiki iliyotangulia.
Alijiuzulu na Bw Mnangagwa, makamu
wa rais aliyekuwa amefutwa kazi wiki iliyotangulia na kutorokea nje ya
nchi, akarejea na kuchukua usukani na kuapishwa Ijumaa baada ya Bw
Mugabe kushurutishwa kujiuzulu.
Credit:BBCSWAHILI
No comments :
Post a Comment