Monday, November 27, 2017

MASAUNI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI NYUMBA MPYA ZA ASKARI POLISI MKOANI MARA


PIX 1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia),akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara,Adam Malima (watatu kulia) na viongozi wengine, baada ya kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na  familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara, kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari hao
PIX 2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano, kukagua nyumba za askari polisi na familia zao zilizopo kata ya Mukonde, Mkoani Mara, Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
PIX 3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, baada ya  kukagua nyumba za  askari polisi na  familia zao zilizopo  kata ya Mukonde, Mkoani Mara,wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano.Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
PIX 4.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, akitoa ufafanuzi juu ya  mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na  familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara kwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
PIX 5
Familia za askari wanaotarajiwa kuhamia katika nyumba mpya zilizopo katika eneo la Mukonde, wakimsikiliza Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati alipotembelea kuona maendeleo ya mradi huo ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani Mara. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments :

Post a Comment