Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Luhaga Mpina katika picha akiongea na wataalam wanahabari na viongozi wa
Wizara hiyo kutoka katika sekta ya Uvuvi, baada ya kuonyeshwa zana
zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu,
katika kanda ya Dar es Salaam.
Katika picha baadhi ya zana
zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa katika oparesheni maalum
ya kupambana na uvuvi haramu katika kanda ya Dar es Salaam.
Kushoto Bw. Obadia Mbogo, Afisa
katika sekta ya uvuvi aliyeshiriki katika oparesheni maalum ya kupambana
na uvuvi haramu, akimuonyesha Waziri Mpina na ujumbe wake aina ya
baadhi ya vilipuzi vilivyokamatwa katika zoezi hilo katika kanda ya Dar
Es Salaam.
……………..
NA MWANDISHI MAALUM
Akiwa katika zoezi la kupongeza
kikosi maalum kilichoanza oparesheni ya kupambana na uvuvi haramau
katika bahari ya hindi leo, zoezi lililokwenda sambamba na kuonyeshwa
vifaa vinavyotumika katika uvuvi haramu vilivyokamatwa katika ...
zoezi hilo
lilioanza mwezi Julai mwaka huu, Waziri wa mifugo na Uvuvi Mhe.
Luahaga Mpana amezitaka halmashauri ambazo shughuli za uvuvi
zinafanyika kutenga fedha ili kuweza kupambana na uvuvi haramu.
Mpina ambaye ameshangazwa na
kitendo cha Halmashauri hizo kukusanya fedha za ushuru zitokanazo na
shughuli na uvuvi na kujisahau kabisa kuingia katika zoezia la kupambana
na uvuvi haramu kwa kutenga fedha hususan za kufanya doria.
Aidha, Mpina Amewataka viongozi
wakuu wa Wizara yake, Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba na Kaimu Mkurugenzi
wa maeneleo ya Uvuvi Bw. Magese Bulayi kutembea na barua rasmi katika
ziara zao za kikazi kwenye halmashauri husika zilizokuwa tayari
kuwawajibisha watumishi wazembe katika zoezi zima la kupambana na uvuvi
haramu.
“Mkurugenzi wa maendeleo ya uvuvi
na katibu Mkuu,nawaagiza mtembee na barua zilizotayari kusimamisha au
kufukuza kazi watumishi wazembe katika halmashauri, barua hizo zibaki
wazi katika sehemu ya kujaza majina yao tuu, na ndani ya mwaka mmoja
nataka tukomeshe kabisa uvuvi haramu. “ Alisisitiza Mpina.
Awali akieleza madhara ya matumizi
ya kitoweo cha samaki waliyovuliwa kwa njia ya vilipuzi na mabomu,
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yohana Budeba alisema kuwa samaki
wanaovuliwa kwa njia hiyo huleta madhara makubwa kwa walaji ikiwa ni
mapoja na magonjwa ya tumbo na Saratani
No comments :
Post a Comment