Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Waziri Mkuu
Mstaafu, Mizengo Pinda, baada ya kuwasili kwenye Mahafali ya 33 ya Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania mjini Singida ambapo alikuwa mgeni rasmi,
Novemba 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
yaliyofanyika mjini Singida Novemba 30, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Chuo
Kikuu hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa (mwenye miwani mbele) akiwa na wahitimu wenzake katika Mahafali
ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika mjini Singida,
Novemba 30, 2017
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akimtunuku Shahada ya
Uzamili Katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera (Master Of Education in
Administration, Planning and Policy Studies), Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Mary Majaliwa (kushoto) katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania yaliyofanyika mjini Singida, Novemba 30, 2017. Wapili kulia ni
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Watatu kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi
na Tekinoloji, Profesa Joyce Ndalichako.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akitelemka kutoka kwenye jukwaa baada ya kutunukiwa Shahada ya
Uzamili Katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera (Master of Education in
Administration, Planning and Policy Studies) na Mkuu wa Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania na Waziri Mkuu MStaafu, Mizengo Pinda (kulia) huku
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akipokea ua kutoka kwa mwanae, Saad Majaliwa Kassim baada ya
kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera
(Master of Education in Administraion, Planning and Policy Studies)
katika Mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika
mjini Singida Novemba 30, 2017.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
……………….
WAZIRI MKUU ATAKA UDAHILI ELIMU YA JUU UONGEZWE
*Ashuhudia mkewe akitunikiwa Shahada ya Uzamili OUT...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema uchumi wa kati na wa viwanda hauwezi kufikiwa au kuwa endelevu
pasipo kuwa na kiwango cha udahili katika elimu ya juu cha angalau
asilimia 23.
“Hivi sasa, kiwango cha
Tanzania cha udahili katika elimu ya juu ni asilimia nne. Kiwango hiki
ni kidogo hata kuliko nchi kama Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo, ambao
licha ya hali ya vita nchini mwao kwa muda mrefu, wamefikia asilimia
saba,” amesema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Alhamisi, Novemba 30, 2017) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji
wa Singida na mikoa jirani waliohudhuria mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania (OUT) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa
Katoliki mjini Singida,
Waziri Mkuu amesema takwimu
zinaonyesha kwamba karibu nchi zote washirika katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki, ukiacha Burundi, zina viwango vya juu zaidi vya udahili
katika elimu ya juu na kwa maana hiyo zimeizidi Tanzania.
Amesema, Chuo Kikuu pekee chenye kanuni za udahili (open entry), chenye kufundisha, kujisomea na hata kutathmini maendeleo ya wanafunzi (assessment on demand) ni Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
“Naungana na Mheshimiwa Rais
kuwaomba mtumie fursa hiyo, kuisaidia nchi yetu kuongeza kiwango cha
udahili wa wananchi wake katika elimu ya juu, kwa haraka na kasi
itakayotuwezesha kufikia lengo la kuwa nchi ya uchumi wa kati na wa
viwanda, ifikapo 2025.”
“Kwa kushirikiana na Baraza la Elimu Masafa Afrika (African Council for Distance Education (ACDE), Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Baraza
la Elimu ya Ufundi (NACTE) na hata vyuo vikuu vingine ndani na nje ya
nchi yetu, ongezeni ubora na panueni wigo wa udahili, kwenye programu za
sasa na zingine mtakazoziongeza,” alisisitiza.
Aliwataka wahakikishe kuwa siku zote, mfumo wao wa utoaji elimu, yaani elimu huria na masafa (Open and Distance Learning (ODL) unajitanabaisha
kama mfumo wa kisasa na mahiri katika kutoa elimu na mafunzo yenye
ubora unaokubalika na kutambulika kitaifa, kikanda na kimataifa.
“Kwa kuzingatia malengo ya
Dira ya Taifa ya Maendelelo na mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano,
napenda nisisitize kuwa dira ya utendaji wenu, ijikite katika maeneo
yaliyoainishwa, chini ya mwanvuli wa kaulimbiu ya Chuo “elimu bora na nafuu kwa wote.”
Waziri Mkuu amesema katika
kutambua umuhimu wa elimu huria na masafa kwa maendeleo ya elimu hapa
nchini, Serikali inaunga mkono azma ya Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia ya kuanzisha dawati maalumu kwa ajili ya kuimarisha Mfumo wa
Elimu Huria na Masafa.
“Kupitia hafla hii, ninaagiza
dawati kama hilo lianzishwe pia katika Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU)
na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa lengo la kuhakikisha kuwa
taratibu zao za ithibati zinazingatia na kukidhi matakwa ya viwango vya
mfumo wa Elimu Huria na Masafa,” alisema Waziri Mkuu.
“Ninaungana na Waziri mwenye
dhamana kuagiza kuwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Taasisi ya Elimu
ya Watu Wazima (TEWW) washirikiane na TCU na NACTE kuhakikisha kuwa
taratibu za ithibati zinatekeleza azma ya Serikali kama ilivyoainishwa
kwenye Sera ya Elimu ya Mafunzo 2014, hususan juu ya suala la kuwatambua
watu waliopata ujuzi bila kupitia mfumo (rasmi) wa elimu na mafunzo,”
alisisitiza.
Waziri Mkuu pia alishuhudia mke wake, Mary Majaliwa akitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera (Masters’ of Education in Administration, Planning and Policy Studies) na Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Waziri Mstaafu, Mizengo P. Pinda.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
- L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, NOVEMBA 30, 2017
No comments :
Post a Comment