Thursday, November 30, 2017

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) UTAENDELEA KUTOA FIDIA BORA – ERIC SHITINDI KATIBU MKUU – OWM



  Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba ya kufunga Mkutano
wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia
kilele leo alasiri kwenye Kituo cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha Novemba
30, 2017.


NA K-VIS BLOG
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Eric
Shitindi amewahakikishia wadau wote wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
kuwa Mfuko utaendelea kutoa mafao bora kwa wafanyakazi wote sekta binafsi na
umma ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Hayo
ameyasema leo Novemba 30, 2017 wakati alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Aidha,
Bw. Shitindi amesisitiza ya kuwa suala la elimu ni la msingi sana na
limejitokeza ambalo mfuko ni lazima uhakikishe umewafikia wadau wote ili
wafanyakazi wote nchini waweze kujua kwa ufasaha haki zao ikiwemo kupata fidia
pale watakapokuwa wanastahili, pia waajiri wao waweze kufuata matakwa ya
kisheria ikiwemo kujisajili na kuwasilisha michango kama kwa wakati.
Pamoja na mambo mengine Bw. Shitindi ameahidi kusimamia zoezi la utoaji elimu
kwa wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ambavyo ilielekezwa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama 
wakati akifungua Mkutano huo tarehe 29 novemba 2017.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira wakati akitoa salamu aliishukuru
Bodi ya Wadhamini pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko kwa kumualika kushiriki
katika Mkutano huo, pia amesema Mkoa wake unavyo viwanda vingi na mashamba
mengi ambavyo vinapelekea kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyakazi ambao watahitaji huduma ya Mfuko.
“Nitawapeni ushirikiano
wa kutosha kuhakikisha waajiri wote wa Mkoa wa Kilimanjaro wanajisajili katika
Mfuko ili  wafanyakazi wasijekukosa Mafao endapo wataumia, kuugua au kufariki” alisema Bi. Nghwira
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Emmanuel Humba, amewashukuru wajumbe
wote wa Mkutano Mkuu kwa kutoa michango mingi ambayo imelenga kuboresha huduma
za Mfuko.
Katika
Mkutano huo uliobeba kauli mbiu ya “Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, umeshuhudia Mfuko ukitoa tuzo kwa waajiri waliofanya vizuri
katika utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.


  Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba ya kufunga Mkutano
wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia
kilele leo alasiri kwenye Kituo cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha Novemba
30, 2017.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Laure Kunenge, akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.

Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Bw. Bernard Konga, (kulia),
akiteta jambo na
Mkurugenzi
Mkuu wa

Mfuko
wa Akiba ya Wafanyakazi
Serikalini (
GEPF) Bwana Daud Msangi wakati wa
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) kwenye
Kituo Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.


 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Emmanuel Humba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi. Radhmina Mbilinyi, wakiongoza kikao.
  Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi. Anna Mghwira, akihutubia Mkutano wa Kwanza wa
Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia kilele leo
Novemba 30, 2017 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha.

 Viongozi wa vyama vya wafanyaakzi wakiteta jambo.

No comments :

Post a Comment