Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais
wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato
walipokutana kwa mazungumzo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi
Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan –JICA nchini
Tanzania Bw. Toshio Nagase, alioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika
hilo Bw. Hiroshi Kato (katikati) walipowasili katika Ofisi za Wizara ya
Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa
pili kulia) wakijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
Tanzania na Japan katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu, nishati,
kilimo na maji, walipokutana Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato akizungumza
kuhusu kuwepo kwa ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Japan katika
suala la Maendeleo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe walioambatana na Makamu wa
Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi
Kato wakifuatiia kwa makini majadiliano kati ya Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na mgeni
wake ambaye ni Makamu wa Rais wa JICA Bw. Hiroshi Kato, Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na
kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Hiroshi Kato (hayupo pichani) katika Ofisi
za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Elijah Mwandumbya akizungumzia
mabadiliko ya Sheria ya Kodi yaliyofanywa hivi karibuni ambayo yanalenga
kutoa misamaha ya kodi yenye tija kwa umma wakati wa Mkutano kati ya
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Makamu
wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw.
Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kamishina Msaidizi wa Sera wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akielezea kuhusu masuala
ya kodi katika maendeleo ya Taifa katika mkutano kati ya Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato
(hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), wa nne kushoto na Makamu wa Rais wa
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa
tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa
waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali ya Japan,
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango
……………….
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
SHIRIKA la Kimataifa la Maendeleo
la Japan (JICA) limesema liko tayari kushirikiana na Serikali kujenga
miundombinu ya kisasa ya...
usafiri, Nishati ya umeme, maji na usafi wa
mazingira katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma.
Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa
Rais wa Shirika hilo Bw. Hiroshi Kato wakati alipokutana na kufanya
mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Jijini Dar
es Salaam.
Bw. Kato alisema kuwa mradi
mwingine wanaotaka kuutekeleza katika mji wa Dodoma ni udhibiti wa taka
ngumu na kwamba wanachosubiri ni Serikali kuainisha maeneo ya vipaumbele
vilivyoko katika mpango mji wa Dodoma.
Aidha Makamu huyo wa Rais wa JICA
alisema kuwa Shirika lake litaendelea kusaidia eneo la kilimo hususan
kilimo cha mpunga ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuwakomboa
wakulima.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango amelishukuru Shirika hilo kwa kuonesha nia ya kusaidia
ujenzi wa mji wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya nchi.
Alisema kuwa mradi huo utasaidia
kwa kiasi kikubwa kuupanga mji wa Dodoma mapema ili kuondoa changamoto
za msongamano wa huduma za jamii kwenye eneo moja kama ilivyo Jijini Dar
es Salaam.
“Pamoja na umuhimu wa miundombinu
ya maji, umeme, usafiri wa mjini, lakini pia tunataka tujenge mapema
njia za juu (ring roads) ili kudhibiti msongamano wa magari” alisema
Dkt. Mpango.
Aliongeza kuwa mradi mwingine wa
kipaumbele katika mji huo ni ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa
katika eneo la Msalato, karibu kilometa 20 kutoka katikati ya mji huo
ili kurahisisha usafiri kwa njia ya anga.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za
Afrika zinazopata ufadhili mkubwa wa miradi mbalimbali ya maendeleo
kutoka Japan kupitia Shirika hilo la Kimataifa la Maendeleo (JICA).
Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa
barabara ya juu (fly over) katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam,
upanuzi wa awamu ya kwanza ya barabara mpya ya Bagamoyo (Mwenge-Tegeta)
na ufadhili mpya wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka
Morocco hadi Mwenge.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia
na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase, pamoja na Maafisa
waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato
Tanzania TRA.
No comments :
Post a Comment