
NA
K-VIS BLOG,ZANZIBAR
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe.January
Makamba amesema moja kati ya changamoto za muungano zilizobakia kwa sasa ni
masuala ya kodi, ikiwemo taratibu za kodi ya VAT na usimikaji wa mitambo
inayoshahabiana kwenye vituo vya forodha vya pande mbili za muungano.
Pia
amesema, kuwepo kwa bandari zisizo rasmi “bubu” ni tatizo linguine na kuziagiza
mamlaka kuhakikisha linasimamia mambo hayo ili kukomesha.
“kumekuwepo
na manung’uniko kwenye eneo hili la ulipaji kodi stahiki na yapo mambo mengi
yanayochangia manung’uniko hayo, nitoe wito tu kwamba lazima tujitahidi
kuhakikisha kero hizo zinaondoka kabisa” alisema Mhe. Makamba
Ameeleza
kwamba amelipokea suala hilo na kwamba tayari linashughulikiwa na mamlaka
husika kwa uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais. Hata hivyo, ameahidi kusukuma
ukamilishaji wà utekelezaji wà masuala haya kupitia kwenye vikao vya ngazi ya
juu kwa maamuzi. Hii ni baada ya kutembelea Shirika La Bandari Zanzibar (ZPC),
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).
Waziri
Makamba leo ni siku ya pili ya ziara yake ya wiki moja kufatilia utekelezaji wa
hatua za kutatua changamoto za Muungano. Ziara ya leo imelenga kubaini
changamoto za kiforodha na kikodi zinazosababisha changamoto katika fursa za
kiuchumi na biashara kati ya wananchi wa pande mbili za Muungano.













No comments :
Post a Comment