NA
WANMM
WIZARA
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendesha warsha ya kuwajengea uwezo
wadau wa masuala ya sekta ya ardhi nchini kuhusu mifumo mbalilmbali
inavyotumika katika kutoa huduma kwa wananchi.
Akifungua
warsha hiyo Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiluka alisema, hadi
sasa wizara inatumia mfumo zaidi ya mmoja kutoa huduma za kila siku kwa
mwananchi. Uwepo wa mifumo hiyo katika
utoaji huduma za sekta ya ardhi ni muhimu kwa ajili ya kurahisisha huduma. Ili
kufikia malengo, ni lazima kuwepo na mfumo mmoja utakaounganisha mifumo yote
hiyo kwa lengo la kuongeza ufanishi na kuboresha huduma.
Uundaji
wa mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (Intergrated Land Management
Information System, ILMIS) unatekelezwa na Wizara ya Ardhi, nyumba na
Maendeleo ya Makazi ikishiriana na wataalamu kutoka kampuni ya IGN FI kwa
udhamini wa Benki ya Dunia. Uundaji huu
ulishaanza na kwa sasa mfumo uko katika hatua ya majaribio.
Dhumuni
kuu la uundaji mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi ni kuimarisha
usalama katika umiliki wa ardhi kwa kuboresha usahihi katika taarifa za ununuzi
ardhi, usajili, upimaji na pia katika kusimamia ardhi kwa ujumla wake.
Utekelezaji
wa Mfumo unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS), utahusisha mambo
mbalimbali kama vile njia rahisi na rafiki ya kusimamia uundaji na uendelezaji
wa mfumo wenyewe, majaribio ya mfumo
katika utekelezaji, ubadilishaji wa taarifa za ardhi zilizopo mfano taarifa za
upimaji na ramani, hatimilki na kuziweka katika mfumo.
Naye
Msajili Msaidizi wa Hati, Appolo Laizer alisisitizia umuhimu wa utumiaji mfumo
unganishi wa taarifa za sekta ya ardhi (ILMIS) kwa wadau wa sekta ya ardhi
alipokuwa akielezea jinsi hatimilki zitakavyotolewa na mfumo huo.
Alisema,
utoaji wa hati kupitia mfumo utaongeza usalama katika nyaraka za umiliki,
huduma sahihi, salama na kwa unafuu zaidi. Mfumo utapunguza muda wa kuhakiki
taarifa katika uhamisho wa milki kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine,
kuongeza ulinzi kwenye maeneo yaliyotengwa kama hifadhi ya barabara, misitu au
maeneo ya wazi.
Utoaji
wa hatimilki kwa kutumia mfumo utasaidia sana kupunguza kama sio kumaliza
kabisa migogoro ya ardhi kwa kulinda umiliki wa mwananchi. Pia mfumo utaondoa
migogoro ya umilikishaji wa hati kwa mtu zaidi ya mmoja pamoja na kuongeza
ulinzi wa hatimilki katika taasisi za kifedha.
Wadau
wa masuala ya sekta ya Ardhi wakisikiliza jinsi mifumo inavyofanya kazi katika
utoaji huduma za Ardhi.
No comments :
Post a Comment