Monday, October 2, 2017

NAIBU WAZIRI MABULA AZUNGUMZIA JUU YA MAKAZI WAKATI DUNIA IKIADHMISHA SIKU YA MAKAZI ULIMWENGUNI


Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akihutubia katika hafla ya maadhimisho ya 32 ya makazi duniani kutoka kulia ni mkurugenzi wa nyumba Bw.Pius Tesha na wa pili kulia ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala maadhimisho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba kulia akitoa salam kwa Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula wa kushoto  katika maadhimisho ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala.


Mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala kushoto akitoa maelezo kwa wadau wa nyumba na makazi katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula na wa pili kushoto ni Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba.


Mkurugenzi msaidizi wa urasimishaji makazi Bi.Beritha Mlonda akiwasilisha makala ya urasimishaji makazi katika maeneo yaliyoko kwenye mkakati wa mpango wa makazi bora kwa Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam hivi leo.


Wadau wa nyumba na makazi wakifuatilia mkutano wa maadhimisho ya 32 ya makazi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo ambapo kauli mbiu ya mwaka  huu ni “sera za nyumba ,nyumba za gharama nafuu”.



Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula, kulia ni mkurugenzi wa mipango miji Profesa John Lupala na kushoto ni Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa nyumba na makazi wa bodi ya mwenge Jijini Dar es Salaam katika madhimisho ya 32 ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo.(PICHA NA PASCHAL DOTTO- MAELEZO)

No comments :

Post a Comment