Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akimlisha keki John
Patrick mteja wa benki ya CRDB ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo cha utumishi wa
Umma Singida, kama ishara ya kuzindua wiki ya huduma kwa mteja katika.
NA MWANDISHI WETU,
SINGIDA
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ameishauri Benki ya
CRDB Mkoa wa Singida kuwasiadia vijana elimu na mikopo ya kutambua na kutumia
fursa zilizopo ili waachane na kauli za kujiita ‘mabomu yanayosubiri kulipuka’.
Dkt Nchimbi ametoa ushauri huo mapema leo wakati akizindua wiki
ya huduma kwa mteja katika benki ya CRDB tawi la Singida huku akisisitiza benki
hiyo kuwa bega kwa bega na Vijana.
“Vijana wetu wasione fahari kabisa kujiita mabomu yanayosubiri
kulipa, Singida tuna fursa nyingi wasibweteke watumie benki hizi na nyinyi
pamoja na benki nyingine jitahidini kuwashika vijana hawa wakipewa elimu ya
ujasiriamali na mikopo wataifikisha Singida mbali kiuchumi”, amesema Dkt
Nchimbi.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Singida umejipanga kuzalisha chakula cha
kutosha ili uweze kulisha makao makuu ya nchi yaani Dodoma hivyo vijana
wabadilike na wawe mabomba ya kusafirishia chakula na bidhaa mbali mbali.
Dkt Nchimbi ameongeza kuwa huduma za kibenki zinawasaidia
watumishi wa umma katika kupanga matumizi ya pesa kwakuwa isingekuwa mishahara
kupitia benki kungekuwa hakuna kinachosalia katika mishahara yao huku hicho
kidogo kinachosalia kinakuwa cha muhimu sana.
Ameongeza kuwa kuelekea uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda
huduma bora za kibenki ni hakikisho la safari hiyo kuwa salama na yenyewe
uhakika huku benki zikiwa ni mahali panapo waunganishawajasiriamali
wakubwa kwa wadogo.
Ameongeza kuwa benki ya Crdb inaaminika ndio maana wajasiriamali
na watumishi wengi wamekuwa wakiitumia hivyo na wateja wao pia wajenge tabia ya
kuaminika hasa kwa kurejesha mikopo yao bila usumbufu.
“Watu wengi wamekuwa wakikopa bila ya kuwa na malengo hivyo
kuishia lawama au hukopa kwa mazoea bila ya kujiandaa nini atafanyia huo mkopo,
mteja wa hivyo anaweza kubadilika na kutokuwa mwaminifu hivyo benki mna jukumu
kubwa la kutoa elimu ya kutosha wateja wenu”, amefafanua Dkt Nchimbi.
Ameeleza kua benki iendelee kuwaelimisha wajasiriamali na
wananchi wengine kuwa kukopa sio aibu na mtu ambaye anakopesheka hiyo ni
heshima hivyo atambue fursa hiyo na kuitumia vizuri.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Singida Innocent
Arbogast ameeleza kuwa benki hiyo inatoa mikopo kuanzia kwa wajasiriamali
wadogo mpaka wakubwa pamoja na kutoa elimu pamoja na huduma za Sim banking,
malkia akaunti na akaunti za watoto.
Arbogast amesema kuwa wiki ya huduma kwa mteja wataitumia vizuri
kwa kuwatembelea wajasiriamali wote mitaani na kuelezea huduma zao kwakuwa wiki
ya huduma kwa mteja ina lenga kuongeza uaminifu kati ya benki na wateja wao.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba
amesema benki hiyo imekuwa ikiwasaidia watumishi ili waweze kutimiza malengo
yao huku watumishi wakiwa waaminifu katika kurejesha mikopo hiyo.
ACP Magiligimba ametoa mfano wake yeye ambaye ameweza kujenga
nyumba kutokana na mkopo wa benki hiyo hivyo watumishi wengine wasione aibu
kukopa ila wawe wamejiwekea malengo mazuri ya matumizi ya mikopo hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikata keki kama
ishara ya kuzindua wiki ya huduma kwa mteja katika benki ya CRDB, Kushoto kwake
ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na anayefuata ni Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba kabla hajamlisha keki
wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa Mteja katika benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB Singida Innocent Arbogast akijiandaa
kumlisha keki Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi wakati wa kuzindua
wiki ya huduma kwa mteja katika benki hiyo.
Wateja wa Benki ya CRDB wakiendelea kupatiwa huduma katika benki
hiyo, huku wiki ya huduma kwa mteja inayolenga kuongeza uaminifu kati ya benki
na wateja wake, ikiwa imezinduliwa.
Wateja wa Benki ya CRDB wakiendelea kupatiwa huduma katika benki hiyo,
huku wiki ya huduma kwa mteja inayolenga kuongeza uaminifu kati ya benki na
wateja wake, ikiwa imezinduliwa
No comments :
Post a Comment