Katibu
Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda akisisitiza
jambo wakati wa Kikao cha Pamoja kati wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) na Mfuko wa Maendelo ya Afrika wa China (CADFUND)
kilichofanyika Shangrila Hotel, Guangzhou China juzi. Kushoto kwake ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bwn. FRANCIS Assenga na kulia kwake ni
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na Afisa Ubalozi wa
Tanzania nchini China Bwn. Lusekelo Gwassa.
PICHA YA
PAMOJA ya baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Ushiriani wa Biashara na
Uwekezaji kati ya China na Tanzania likilofanyika Guangzhou China Oktoba
2017. Katikati ni Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof.
Adolf Mkenda aliyekuwa Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo, kulia kwake ni.
Mhe. Adam Kimbisa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki; Katibu Mkuu wa
Biashara Viwanda na Masoko wa Zanzibar Bw. Juma Alli Juma; Balozi wa
Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki; na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa
Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Akaro. Kulia kabisa aliyesimama ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TADB) Bw. FRANCIS
Assenga.
Kutoka
kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB) Bwn. FRANCIS Assenga, Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na
Uwekezaji Bwn. ADOLF Nkenda; Makamu Rais na Naibu Mtendaki Mkuu wa
CADFUND Bwn. Wang Yong na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa
Kairuki, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja
Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya mazungumzo na Taasisi mbili muhimu za kifedha na kiuchumi nchini China kwa ajili ya upatikanaji wa fedha za uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na viwanda nchini Tanzania hususan kwenye Sekta ya Kilimo.
Majadiliano hayo yalifanywa kati ya Ujumbe wa TADB ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki , Bw. Francis Assenga alipokutana na Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya China (CBD) kwenye Mkutano uliofanyika Shangrila Hotel, Guangzhou China wakati wa Kongamano la Pamoja la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Pande zote mbili zilikubaliana kuendelea na kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kupatikana kwa fedha kwenye uwekezaji wa miundo mbinu ya kilimo na viwanda vidogo vidogo vya uongezaji thamani kwenye mazao ya kilimo kwa wakulima nchini.
Katika ziara hiyo TADB pia ilifanya majadiliano ya kina na Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa China (China African Development Fund) ambao hufanya uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na ya kibiashara (Equity investmenta) kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Ujumbe wa ulioongozwa na Makamu Mtendaji wa Rais na Naibu Mtendaji Mkuu wa 'CADFUND' Bwn. Wang Yong aliyefuatana na Mkurugenzi Mkuu wa Sekta ya Viwanda, Kilimo, Afya na Uwekezaji, Bw. Lei Ma; Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Masoko na Huduma Elekezi Bw. Henry Liu; na Meneja wa Uwekezaji wa Viwanda, Ardhi na Kilimo Bw. Luo Zhongquan.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji (UWEKEZAJI), Prof. Adolf Mkenda. Wengine waliohudhuria ni Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki; na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini China Bw. Lusekelo Gwassa.
Katika mazungimzo hayo, pamoja na mambo mengine CADFUND walikubali kuendelea kutoa fedha kwenye miradi ya kiuchumi na uwekezaji mkubwa kwenye nyanja kuu nne zikiwemo kilimo; viwanda; madini; na miundombinu kama ya maji na umwagiliaji.
Aidha CADFUND na TADB ziliainisha maeneo kadhaa ya ushirikiano kama vile Uhakiki na Usimamizi wa miradi; Utafiti; Ukaguzi; na Ujengaji wa Uwezo.

No comments :
Post a Comment