Friday, October 20, 2017

KOCHA WA ARSENAL ARSENE WENGER ATAMBIA MAFANIKIO YA LIGI YA UROPA

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema timu yake imeonyesha uwezo kwa kuendelea kufanya vizuri Ligi ya Uropa baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Crvena Zvezda huko Serbia.

Shujaa wa mechi hiyo alikuwa mshambulia Olivier Giroud aliyefunga goli kwa tik-taka katika dakika za mwisho dhidi ya Crvena Zvezda iliyobakia na wachezaji 10, na kuifanya kushinda mechi tatu katika kundi lao la H.
        Olivier Giroud akiwa ameanguka chini baada ya kuupiga mpira uliozaa goli kwa staili ya tik-taka
          Mchezaji wa Crvena Zvezda Milan Rodic akipewa kadi nyekundu ndani ya dakika 10 tu za mchezo huo

No comments :

Post a Comment