NA K-VIS BLOG,
KISARAWE
MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewapongeza wananchi wa kisarawe kwa
ushirikiano mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa,
Ofisi za walimu, nyumba, pamoja na vyoo.
Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akikagua mradi ya ujenzi wa
madarasa wilayani kisarawe katika vijiji vya Mitengwe, Kitonga, Boga, na kwala.
Katika vijiji hivyo, Jafo alikagua ujenzi wa vyumba vipya vya
madarasa 15, Ofisi za walimu 4, pamoja na matundu ya vyoo 40 ambapo ujenzi wake
unafanyika kwa bora unaotakiwa.
Kutokana na mwamko mkubwa ulioonyeshwa na wananchi hao katika
kushirikiana na serikali na viongozi walio wachagua akiwemo mbunge na madiwani
wote wa kisarawe, Jafo amesisitiza wananchi wengine katika wilaya mbalimbali
kushirikiana na serikali pamoja na viongozi wao ili kujiletea maendeleo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiipongeza
kamati ya ujenzi kijiji cha Kwala wilayani Kisarawe kwa ujenzi wa madarasa
mapya.
Baashi ya matundu ya vyoo yaliyokamilika kujengwa wilayani
Kisarawe.
Diwani wa kata ya Mzenga Mohamed Lubondo(katikati) akiwa na
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi
wa madarasa na vyoo katika shule ya msingi Mitengwe wilayani Kisarawe.
Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Mitengwe
wilayani Kisarawe.
No comments :
Post a Comment