Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, "Mzee Rukhsa"
akizungumza na wazee wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017 .
NA WAMJW
Vijana nchini wameshauriwa kujitolea na
kuwatunza wazee katika maeneo yao ili kupata ushauri na busara za wazee hao kwa
maendeleo yao na taifa.
Hayo yamesemwa Mjini Dodoma na Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wazee katika
kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kila Oktoba Mosi
ya kila mwaka.
Mhe. Mwinyi amesema kuwa jukumu la kuwatunza na
kuwalea wazee sio la Serikali pekee bali jamii pia ina nafasi yake katika
kuwatunza wazee hasa Vijana.
Mhe. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali imejitaidi sana
kuweka mazingira mazuri kwa wazee kwa kuwapatia huduma za Afya na kuwatunza
wazee wote ambao hawana ndugu wa kuwatunza katika makambi mbalimbali ya wazee
nchini.
“Niwaombe vijana mtutunze sisi wazee kwani na sisi
tulikuwa vijana kama ninyi na mkiweka utamaduni huu utawasaidia na ninyi mkiwa
wazee hapo baadae” alisema Mhe. Mwinyi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, MAendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Mstaafu Mhe.
Mwinyi kuwa Serikali itaendelea kuwatunza wazee nchini na kuhakikisha wanapata
hudumu zote muhimu.
“Nikuhakikishie Mhe. Mwinyi kuwa tutaendelea kuwatunza
wazee kwa kuwapatia huduma muhimu hasa huduma za Afya” alisema Mhe. Ummy.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee nchini Mzee
Sebastian Bulegi amemuomba Mhe. Mwinyi kufikisha shukurani zao kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa moyo wake
wa kuwajali wazee nchini.
“Mhe. Mwinyi naomba utufikishie shukurani zetu kwa
Mhe.Rais Magufuli kwa kutujali wazee hasa kwa kutatua changamoto zetu
zinazotukabili” alisema Mzee Sebastian.
Siku
ya Wazee Duniani huadhimishwa Oktoba Mosi kila mwaka kufuatia Azimio la
Umoja wa Mataifa linalozitaka nchi wanachama kutenga siku maalumu ya kutafakari
mchango wa Wazee katika maendeleo ya jamii na kuwaenzi ili wawe na maisha
bora na yenye matumaini na Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “
Kuelekea uchumi wa Viwanda:Tuthamini Mchango, Uzoefu na Ushiriki wa Wazee kwa
maendeleo ya Taifa”.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa
salamu za Mkoa kwa Mgeni Rasmi wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwapungia mkono wazee wakati
wakiingia kwa maandamano kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani iliyofanyika katika
viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya
Wazee ya Mwaka 2003 kwa Mgeni wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya
Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya
Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi (hayupo Pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya
Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi (hayupo Pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
No comments :
Post a Comment