RAIA wa Rwanda, wamepiga kura leo
Agosti 4, 2017 kumchagua rais wao, amba[o wadadisi wa mambo wanabashiri
kuwa Rais aliye madarakani, Paul Kagame(pichani) ataibuka mshindi na
hivyo kushika madaraka kwa kipindi cha tatu cha miaka saba.
Uchaguzi huo umeripotiwa kufanyika
katika hali ya utulivu na kwa mara ya kwanza umeshirikisha wagombea
wengine wa upinzani Bw. Frank Habineza kutoka chama cha kijani (Green
Party) na mgombea huru Bw.Philippe Mpayimana.
Rais Kagame amesifika kwa kurejesha
utulivu kwenye taifa hilo dogo lenye idadi ya watu zaidi kidogo ya
milioni 10 baada ya kushuhudia mauaji ya halaiki ya mwaka 1994, ambapo
watu wanaofikia milioni moja waliuawa katika mapigano ya kikabila
kufuatia majeshi ya RPF yaliyokuwa yakiongozwa na Kagame wakati huo
akiwa kiongozi wa vita vya msituni kumng'oa Rais wa wakati huo Juvenal
Habyarimana.
Mauaji hayo yaliibuka muda mfupi baada ya ndege iliyowachukua Rais Habyarimana na mwenzake wa Burundi Cyprien
Ntaryamira, kudungukiwa wakati ikijianmdaa kutua kwenye uwanja wa ndege
wa Kigali. Marais hao walikuwa wakitokea jijini Arusha kuhudhuria
mazungumzo ya kuleta amani kwenye mataifa hayo mawili ya Rwanda na
Burundi.
Rais Kagame an chama
chake cha RPF, aliingia madarakani na kwa kiasi kikubwa Rwanda imekuwa
tulivu tangu achukue mamlaka ya uongozi licha ya malalamiko ya hapa na
pale ya kwamba anakandamiza upinzani na hataki kukosolewa.
Wafuasi wa Rais Kagame wakiserebuka wakati wa mikutano ya kampeni
Bw. Frank Habineza mgombea kutoka chama cha upinzani Green Party.
Mgombea huru Bw.Philippe Mpayimana.
Mwananchi wa Rwanda kipiga kura yake mapema leo Agosti 4, 2017
Kwa utulivu kabisa wananchi wakiwa kwenye foleni tayari kupiga kura leo asubuhi Agosti 4, 2017.
No comments :
Post a Comment