NA
K-VIS BLOG/MASHIRIKA YA HABARI
ULAYA Kusini imekumbwa na joto kali
linalofikia nyuzi joto 40c, ambapo kisiwa cha Cicily ndio kimeathirika zaidi.
Tayari Uingereza imeonya raia wake
wanaosafiri katika kipindi cha mapumziko, kuchukua tahadhari kufuatia hali hiyo
mbaya ya hewa kuwahi kulikumba bara la Ulaya.
Kwa mujibu wa mashirika ya habari
ya kimataifa, Ufaransa, Ugiriki, Italia, Croatia na baadhi ya miji ya
Ulaya mamlaka za hali ya hewa za miji
hiyo zimeripoti kiasi cha joto kumepanda hadi kufikia nyuzi joto 47c na hali
hiyo pia imeripotiwa kwenye baadhi ya nchi za Asia kama vile China. Italia imeiita hali hiyo kama “Heatwave
Lucifer na nchi 11 wameiita hali hiyo ya hewa kuwa ni ya hatari katika nchi za
Serbia, Hungary, Croatia na Poland.
No comments :
Post a Comment