Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WAZIRI
wa mambo ya ndani ya nchi ,Mwigulu Nchemba ,amewataka askari wa
uhamiaji nchini kuhakikisha wanataifisha magari na vyombo vya... usafiri
wanavyokutwa navyo wahamiaji haramu ,wakati wanapokamatwa.
Aidha amewaagiza askari hao kuwakamata watu wanaowalipia faini wahamiaji haramu na kuwafungulia mashitaka.
Mwigulu aliyasema hayo,wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa
ofisi za mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na ofisi mpya ya
uhamiaji ya mkoa wa Pwani ambazo zote zipo wilayani Kibaha.
Alisema
endapo magari na vyombo vinavyosafirishia wahamiaji haramu ikiwemo boti
vitaifishwe na kutumika katika kazi za ujenzi wa taifa.
“Haiwezekani
mtu aingie nchini kwa makusudi ,bila kibali halafu inapotakiwa kulipa
faini kutokana na kosa hilo atokee mtu kuwalipia faini kwa haraka jambo
linalosababisha vitendo hivyo kuenea kwa kasi”alisema Mwigulu.
Mwigulu
alieleza kwamba,ni lazima iangaliwe,jamii inapaswa kujiepusha na
kushirikiana na kundi hilo ili kupunguza wimbi kubwa la wahamiaji haramu
nchini.
Waziri
huyo alisema ,iangaliwe njia za kudhibiti wahamiaji hao pale
inapotokea kukamatwa ama kushtakiwa na kuhukumiwa pasipo kuwalinda kwa
kuwalipia faini.
“Mkiwakamata
pia na magari myataifishe siku hiyo hiyo na kuyapeleka magereza ili
yakabebe mawe,na hata mkiwakamata kwenye boti taifisheni hizo boti
hakuna kuweka viporo”alisema Mwigulu.
Awali akitembelea ofisi mpya katika jengo la
vitambulisho vya taifa (NIDA),Mwigulu aliwaagiza watendaji wa ofisi
hiyo kuhakikisha wanafanyia kazi agizo la dk.John Magufuli la
kuunganisha utambulisho wa jumla kwa wananchi.
“Wananchi wanatakiwa wawe na utambulisho wa aina moja pekee unaojumuisha taarifa zao zote”alisema alisisitiza Mwigulu.
Nae
afisa Uhamiaji Mkoani Pwani ,Plasida Mazengo alisema ofisi yake
inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vitendea kazi
hali inayosababisha kufanyakazi kwenye mazingira magumu .
Alimuomba
waziri huyo kuangalia namna ya kusaidia kutatua changamoto hizo ili
waweze kufanya kazi zao kifanisi zaidi kwa maslahi ya watanzania.
Kaimu mkurugenzi wa uzalishaji vitambulisho (NIDA) Alfonce Malibiche alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 99.9 .
Kaimu mkurugenzi wa uzalishaji vitambulisho (NIDA) Alfonce Malibiche alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 99.9 .
Na utakapokamilika utawarahisishia wananchi kupata huduma kirahis,na jengo litaanza kazi rasmi mwishoni mwa mwezi huu .
No comments :
Post a Comment