Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, (kushoto) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, wakisalimiana na Mhe. Nguyen Xuan Phuc, Waziri Mkuu wa Vietnam |
NA
MWANDISHI MAALUM, VIETNAM
LEO
Agosti 2, 2017, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yao nchini Vietnam, Mhe. Charles
Mwijage, (Mb.) Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mhe. Dkt. Charles
Tizeba, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wamekutana kwa... mazungumzo na Mhe.
NGUYEN XUAN PHUC, Waziri Mkuu wa Vietnam ambapo walijadili namna ya kuimarisha
mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi na biashara baina ya nchi hizo mbili.
Mazungumzo hayo yalifanyika mara baada ya kukamilisha kongamano la tatu la
biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietnam lililofanyika siku hiyo hiyo
ya tatu ya ziara yao.
Katika
mazungumzo yao, Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Vietnam aliipongeza Serikali ya
Tanzania kwa hatua nzuri za kiuchumi inazoendelea kupiga kwa kuzingatia kwamba
Tanzania ni kati ya nchi kumi duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi na ni
ya kwanza kwa Afrika Mashariki. Aliishukuru pia serikali ya Tanzania kwa
kuendelea kuisaidia kampuni ya Halotel katika utoaji wa huduma zake za
mawasiliano na hasa vijijini. Aliwakikishia Washemiwa Mawaziri hao kuwa Vietnam
itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinafikia
malengo ya biashara yaliyowekwa na Waheshimiwa Marais wa nchi hizi hapo mwaka
2016 nchini Tanzania.
Kwa
upande wake Mhe. Mwijage alieleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua na kuenzi
urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Alieleza kuwa
lengo la ziara hiyo ni kuendeleza mikakati ya kutekeleza maelekezo ya viongozi
wa nchi hizo mbili kwamba ifikapo mwaka 2020 biashara kati ya nchi hizi ifikie
dola za marekanii bilioni 1. Hivyo, kongamano la uwekezaji lililofanyika hapo
mjini Hanoi, limeweza kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania wapatao 30 na
wafanyabiashara wa Vietnam zaidi ya 200. Aidha, kutokana na kongamano hilo,
changamoto mbalimbali zilielezwa ambazo zinarudisha nyuma jitihada za
wafanyabiasha. Alieleza kuwa tayari amekutana na Waziri wa Biashara na Biwanda
wa Vietnam na wamekubaliana timu ya wataalmu ikutane Dar es Salaam mwezi
Septemba kuanza kufanyia kazi mapungufu hayo kwa pande za nchi zote.
Nae
Mhe. Tizeba alimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa nafasi aliyowapa ya kukutana
pamoja na kuwa ana majukumu mengi. Alieleza kuwa changaoto nyingi zilizoelezwa
na wafanyabiashara katika kongamano la biashara zingeweza kutatuliwa iwapo hati
za makubaliano zilizopendekezwa na nchi hizo zingekuwa zimekamilishwa na
kuwekwa saini. Hivyo, alimuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu asaidie kwa upande wa
Serikali ya Vietnam ili hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya taasisi
mbali mbali za Tanzania na Vietnam zikamilishe na kurahisisha biashara.
No comments :
Post a Comment