Tuesday, August 1, 2017

MAADHIMISHO YA NANENANE 2017 KITAIFA KUFANYIKA LINDI KUANZIA KESHO

Na Mathias Canal, Lindi
   
Maonesho ya Kilimo (NaneNane) yanataraji kuanza kesho Agosti 1, 2017 kote nchini kwa ngazi mbalimbali za kanda huku Maonesho hayo Kitaifa yakifanyika Mkoani Lindi huku Maandalizi na maonesho ya  Ki-Kanda yanaratibiwa na uongozi wa  mikoa husika.

Maandalizi ya Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane yatafanyika kwa siku 8 ambapo Kitaifa yatafika ukomo jioni ya Agosti 8, 2017 katika Viwanja vya Ngongo na Maeneo mengine yatakapoadhimishwa kikanda  katika  viwanja vya maonesho ni John Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere –Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni -  Dodoma; Nyahongolo – Mwanza; na Fatuma Mwassa - Tabora. 

Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo hutoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini. 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg Mathew Mtigumwe wakati akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com  kueleza muktadha wa Maonesho hayo ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi na kubebwa na kauli mbiu mahususi kwa mwaka huu 2017 isemayo "Zalisha kwa Tija Mazao ya Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati" 

Mtigumwe ameuambia Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com kuwa Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo wataendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.

Malengo ya maonesho hayo ni utoaji elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi.

Teknolojia/Bidhaa zitakazooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa ambapo piaTaasisi za kitafiti ambazo zitaonyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa.

Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.

Maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yohusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yalifunguliwa tarehe 03 Agosti 2016 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe.

Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane ina sherekewa nchini kote tarehe 8 Agosti kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo.

Miaka ya 1990 sherehe hizi zilikuwa zikifanywa tarehe saba Julai kila mwaka na kuzingatia mafanikio makubwa na changamoto zinazokabili sekta ya kilimo inayowashirikisha wadau wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa.Ambapo Lengo la serikali likawa kuitumia Saba Saba kama siku ya maonyesho ya biashara ya kimataifa, ambapo wafanyabiashara wengi walijitokeza ama hujitokeza kuonyesha bidhaa zao wanazozalisha na siyo kuwafundisha Watanzania mbinu za kuzalisha biadhaa hizo.

Picha zaidi zinaonyesha maandalizi ya Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo.
……………………………………………………………………

Na Fredy Mgunda, Mafinga

Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka ...Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi.
“Tulikuwa hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka unaoanza tutakusanya mapato na kukuza mapato kutoka asilimia 56 hadi kuvuka lengo la serikali la asilimia 80” alisema Makoga
Makoga aliwataka wananchi na viongozi kushiriana kukusanya mapato kulingana vyanzo ambavyo madiwani wameviolozesha kwa manufaa ya halmashauri ya Mafinga Mjini ambavyo vipo kisheria kutoka serikali kuu.
Jamani naombeni mchango wetu kufanikisha swala hili la kukusanya mapato ili tufikie lengo la serikali kwa kuwa mwaka huu hatufikia lengo hilo ni aibu kubwa kwa serikali hii ya awamu ya tank ambayo inaenda kwa kasi kubwa kwa kukuza uchumi wa nchi.
Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa mafinga Zacharia Vang’ota wa kata changarawe,Chesco lyuvale wa Kata ya kinyanambo walimtaka Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuzisimamia ipasavyo sheria ambazo zimetungwa na halmashauri pamoja na serikali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Dr John pombe Magufuli ili kukuza mapato katika halmashauri hiyo.
“Ukiangalia hapa Mafinga tunavyanzo vingi vya mapato lakini watalaamu wetu hawavifanyii kazi ndio maana sisi madiwani tumeamua kuanzia sasa vyanzo vyote tulivyovibainisha leo kwenye baraza vifanyiwe kazi haraka sana ili kukuza mapato ya halmashauri yetu”walisema madiwani
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Mafinga Mjini walisema kuwa Mji huo una changamoto nyingi hivyo serikali ya mji inatakiwa kuanza kuzitumia hizo sheria Mpya haraka ili hata wananchi wayatambue maeneo yanayopaswa kulipa kodi na kuewezesha halmashauri kukuza mapato na kutatua changamoto za Mji wa Mafinga.
“Angalieni nyie waandishi Mafinga maji ni tatizo kubwa,Barbara bado hazijatengenezwa hasa huku mitaani kwetu,Mji bado mchafu kila mtu anatupa takataka anavyotaka kwa kuwa hakuna mtu wa kumkamata ila ukiangalia sheria Mpya zipo lakini hazifanyiwi kazi na Mafinga maeneo ya maegesho ya magari hayalipiwi wakati miji mingine ni moja vya mapato hivyo viongozi wanapaswa kuanza kuzitumia sheria Mpya” walisema wananchi

No comments :

Post a Comment