Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na wafadhili wa mradi wa maji wa Mhande kutoka Canada. |
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na wafadhili wa mradi wa maji wa Mhande kutoka Canada.
Wananchi wa Mhande wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Chritine Mndeme katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kijiji hicho.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma
Christine Mndeme pamoja na Father Fransis wakifungua bomba la maji kama
ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mhande.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na akina mama wa kijiji cha Mhande
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akisalimiana na father Fransis
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akiteta jambo na Brother Anthony ambaye ni muasisi wa mradi wa CPPS.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akikagua eneo la pampu ya maji ya mradi wa maji wa Mhande.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akicheza ngoma baada ya kuzindua mradi wa maji
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhande
……………………………………………………………..
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini
Christine Mndeme leo amezindua mradi wa Maji katika kijiji cha
Mhande,Kata ya Ngh’ong’hona ambao umefadhiliwa na Shirika shirika la
wamishionari wa damu takatifu ya Yesu(CPPS) uliogharimu kiasi cha
Sh.Milioni 35.
Mradi huu umetokana na maombi ya
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa Shirika la hilo
kusaidia kutatua changamoto ya Maji katika kata hii ya Ngh’ongh’ona
ambayo wananchi wake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo kubwa la
upatikanaji maji safi na salama.
Akizungumza katika uzinduzi huo,
Mndeme amelishukuru shirika hilo la CPPS kwa ufadhili wa mradi huo na
kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa kuwa
mstari wa mbele kutatua kero za wanachi wake hususani kero kubwa ya Maji
katika kata ya Ngh’ongh’ona.
Amesema kutatuliwa kwa kero hiyo kumewatua kina mama ndoo kichwani kwa kuwa walikuwa wakienda kuchota maji umbali mrefu.
“Mwili unahitaji maji
unapotafuta maji mbali roho inasononeka hata muda wa kusali unaukosa,
tunashukuru sana shirika hili lakini wananchi tuna wajibu wa kuutunza
mradi huu ambao ni wa thamani kubwa sana,”amesema
Hata hivyo amesema hatasita
kuwachukulia hatua watu watakaoharibu miundombinu ya mradi huo wa maji
huku akiwataka kuunda kamati ya maji ili kuendesha mradi huo.
Aidha amesema kwa kushirikiana
na Mavunde watashughulikia upatikanaji wa umeme katika mradi huo wa maji
ili uweze kutoa huduma ipasavyo kwa wananchi.
Naye, Diwani wa Kata hiyo
Philipo Nangu amesema wananchi hao wamekuwa wakipata adha kubwa ya maji
na kulazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma
hiyo vijiji jirani jambo lilosababisha kushindwa kufanya shughuli za
kimaendeleo.
Kadhalika, Mavunde amesema
amefanikiwa kupata ufadhili wa Shirika la GIZ la Ujerumani ambao
watasaidia kusambaza huduma hiyo ya maji katika kata yote ya
Ngh’ong’hona ili kumaliza changamoto ya Maji kwenye eneo hilo.
No comments :
Post a Comment