| Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania Amin Habib akihutubia wageni waalikwa katika ya hafla ya kununua oparesheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin nchini. |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania Amin Habib akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya kununua oparesheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin nchini. |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania Amin Habib, akiongea Na Distributors wa Arusha kuhusu ununuaji wa operasheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin. |
| Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya kununua oparesheni za Kampuni ya Rangi ya Sadolin nchini |
NA MWANDISHI WETU
Arusha:
Kampuni ya Kansai Plascon Afrika ltd. Ambayo ni kampuni tanzu ya
kampuni ya rangi ya Kansai iliyoko Japan, imehitimisha makubaliano yake
ya... kununua shughuli za rangi za Sadolin nchini Tanzania na nchi nyingine
za Afrika Mashariki. Hii ilitangazwa na Deodatus Makumpa Meneja wa
Kanda ya Kaskazini, Plascon Tanzania wakati akitoa taarifa kwa vyombo
vya habari katika Hotel ya Arusha Jijini Arusha
Kampuni ya rangi ya Kansai ni kampuni ya kimataifa ambayo inaendesha
shughuli zake nchini Japan, China, Mashariki ya Kati, Ulaya na Afrika.
Bidhaa zake inazotoa zinajumuisha upambaji, Viwanda, rangi za kulinda na
mitambo, ina vituo vya utafiti na maendeleo nchini Japan, India na
Afrika Kusuni.
“Tumefurahishwa na mafanikio haya. Kupitia haya, tutaweza kutumia nembo
yenye nguvu ya urithi wa Kansai, uwezo wa kimataifa wa kiufundi, na
utendaji wa kuaminika, kutupatia uwezo mpya, kuweza kupata teknolojia
mpya na utambuzi ambao ni muhimu zaidi katika kuendelea kukuza nembo
hii,” alisema Makumpa
Akiongea kuhusu sababu za kuinunua, Gary van der Merwe, Rais wa Kampuni
ya Plascon Afrika Mashariki alisema kwamba makubaliano haya
yanadhihirisha nia ya Kansai Plascon katika kujiendeleza zaidi duniani.
“Afrika Mashariki ni moja kati ya ukanda ambao unakuwa haraka zaidi
kiuchumi barani Afrika. Kwa ukuaji wa kasi wa daraja la kati, kuongezeka
kwa nguvu ya utumiaji na kukua kwa miji, huu ni muda muafaka wa
kuingiza sokoni bidhaa zetu mbali mbali kwaajili ya kuboresha zaidi
mtindo wa maisha yao wakati huo huo tukiwa tunaongeza kuenea kwetu
duniani”.
Ununuzi huu hautakuwa na mabadiliko katika uongozi wa juu na nafasi
zozote zingine katika kampuni ya Sadolin. Kampuni itaendelea kufanya
shughuli zake kama ambavyo ilikuwa ikifanya kwa kutumia wafanyakazi
waliopo. Amin Habib ambaye anakalia kiti cha Mkurugenzi Mtendaji amesema
kwamba ununuzi huu utapelekea katika matokeo bora na ufanisi zaidi
ambao utanufaisha kampuni hii ya rangi. Kuanzia katika teknolojia mpya
na iliyoboreshwa kutoka katika kampuni ya rangi ya Kansai ambayo ni
kampuni ya kumi ya rangi duniani.
Tangu ianzishwe mwaka 1967 nchini Tanzania, kampuni ya rangi ya Sadolin
imekua na kuwa kampuni kubwa zaidi ya uzalishaji wa rangi, ikiwa
inajivunia zaidi ya 50% ya soko katika rangi za kulinda naza
kutengenezea magari.
Amin Habib amewahakikishia wateja kwamba mabadiliko haya hayatakuwa na
athari zozote katika utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za kampuni
uliopo sasa. Lakini mabadiliko yanakuja na mbinu bora za uendeshaji
kwaajili ya kuwahudumia vyema wateja, kwa ufanisi zaidi na kwa bidhaa
zenye kiwango ambazo hawakutarajia.” Wauzaji wetu wote, Maghala na
maduka yatabakia kuwa wazi kuwahudumia kwa bei ile ile nzuri ambayo
wamekuwa ukiifurahia kwa miaka mingi. Katika miezi michache ijayo,
tukiwa tunakamilisha mabadiliko, tutaanza kuingia katika kutekeleza
makubaliano ya mkataba, kumalizia bidhaa zenye nembo ya Sadolin kutoka
katika maghala yetu na kuwasisitiza wateja wetu kuuliza bidhaa zenye
nembo ya Plascon kutoka kwa wauzaji wao”
Kwa kutambua kwamba kununua na kujiunga kwa makampuni huja na hali ya
kutokuwa na uhakika katika mtazamo wa raslimali watu na mtazamo wa
kiuendeshaji, Gary van der Merwe alisema kwamba kwa kuwa Sadolin kama
biashara tayari ilikuwa inaendesha shughuli zake kwa ufanisi, mkakati
utakuwa ni kuboresha zaidi na kuongeza katika uendeshaji uliopo ili
kuboresha ufanisi.
“Tutafanya kazi ya kupanua zaidi teknolojia ya hali ya juu iliyopo
ambayo tumeikuta ikiwa inafanyakazi. Lengo letu litabakia katika
kuwekeza katika teknolojia ya kiwango cha juu kuwapa wateja wetu rangi
za kiwango cha juu zaidi katika soko.” Alisema.
Lengo letu ni kudumisha nafasi yetu kama wazalishaji wa rangi
wanaoongoza Tanzania na Afrika Mashaririki kwa kuendelea kuboresha ili
kuweza kufikia mahitaji ya wateja wetu yanayobadilika kila siku na
kubakia washindani katika soko. “Soko la Tanzania wanaweza kutarajia
kuanza kutumia application ya simu ya Plascon Visualizer, ambayo
itawaruhusu watu kucheza na kufanya majaribio ya rangi kwaajili ya
nyumba zao na miradi yao kabla ya kwenda kwa wauzaji kutoa oda zao.”
Sadolin imefurahia nafasi yake na kushikilia soko la rangi katika kanda
hii. Ununuzi huu utaongeza mapato ya Kansai Plascon na nafasi yake kama
ambavyo inataka kuimarisha nafasi yake kama kampuni ya rangi inayoongoza
Afrika.
No comments :
Post a Comment