
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa
Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo
katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
NA VERONICA KAZIMOTO
WITO umetolewa kwa viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla
kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi watakaopita maeneo mbalimbali nchini
kukusanya taarifa kwa ajili ya Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo
yaliyofanyika leo mkoani Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga, (pichani juu), amesema utafiti huo ni muhimu katika kunusuru
kaya maskini nchini hivyo haina budi viongozi na wananchi kutoa ushirikiano kwa
Wadadisi wa utafiti husika.
"Kwa namna ya pekee nawaomba Makatibu Tawala wa Mikoa na
Wilaya, Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri, viongozi wa kata na vijiji na
wananchi wote kwa pamoja mtoe ushirikiano wa hali ya juu kwa Wadadisi
watakapokuwa katika maeneo yenu wakikusanya taarifa za utafiti huu",
amesema Mwamanga.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina
Chuwa amesema lengo la kufanya mafunzo hayo ilikuwa ni kuwawezesha Wadadisi
kufahamu taratibu zote zinazohusu kazi ya ukusanyaji taarifa na mbinu
zinazotakiwa ili kupata taarifa sahihi kutoka kwenye kaya mbalimbali nchini.
Jumla ya Wadadisi 85 wamemaliza mafunzo ya siku 20 ya Utafiti wa
Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini yaliyoandaliwa na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na TASAF.
Mmoja wa Wadadisi Maro D. Maro akitoa neno la
shukrani wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa
Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti
mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani
Dodoma.
Baadhi ya Wadadisi na Wasimamizi wakimsikiliza
kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
(hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya
Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi
Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango
mkoani Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA
KAZIMOTO)
Baadhi ya Wadadisi na Wasimamizi wakimsikiliza
kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
(hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya
Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi
Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango
mkoani Dodoma.




No comments :
Post a Comment