|
NA
JESHI LA POLISI NCHINI
MKUU
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa
ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji
wa Jeshi hilo hatua ambayo italiwezesha kufanyakazi zake kwa weledi katika
kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.
IGP
Sirro, amefanya ziara hiyo ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa
kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na
maofisa ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.
Katika
mazungumzo yake IGP Sirro, amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa
kutenda haki na bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha
upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.
Hata
hivyo, katika mabaraza ya kuzungumza na askari na maofisa baadhi ya hoja kadhaa
ziliibuliwa kwa baadhi ya askari waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao, ambapo
IGP Sirro aliahidi kuzishughulikia mapema ili kuzidisha morari katika
utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Aidha,
katika ziara yake IGP Sirro, alipata fursa ya kukutanana Wajumbe wa Kamati za Ulinzi
na Usalama ya mkoa huku masuala kadhaa ya kiusalama na mbinu na mikakati
ikijadiliwa katika kamati hizo na kuahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha
kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu.
|
No comments :
Post a Comment