
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM
Rose Tweve akizungumza na madiwani na wananchi wa halmashauri ya Mafinga
Mjini wakati wa baraza la madiwani

Mwenyekiti
wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa
baraza la madiwani lilofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo
Baadhi
ya madiwani,viongozi pamoja na wananchi waliohudhuria baraza la
madiwani lilofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mafinga Mjini.
Na fredy Mgunda, Mafinga.
Mbunge
wa viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Rose
Tweve amewata watendaji wa halmashauri ya Mafinga Mjini kufanya kazi kwa
kujituma na kuwa
tumikia wananchi wa Jimbo la Mafinga Mjini ambalo linaongozwa na mbunge Cosato Chumi.
tumikia wananchi wa Jimbo la Mafinga Mjini ambalo linaongozwa na mbunge Cosato Chumi.
Akizungumza
wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Mafinga Mjini alisema
kuwa watendaji wengi wamekuwa wakilalamikiwa kutokana na kufanya kazi
chini ya kiwango na kuwapelekea wananchi kuwa na changamoto ambazo
hazina sababu.
“Hivi
watendaji kitu gani kinachosababisha msifanye kazi kwa weledi kama
ambavyo mlivyokuwa mnaomba kazi,jamani serikali ya awamu ya tano haitaki
mfanye kazi kwa mazoea kama zamani saizi mnatakiwa kufanya kazi
kutokana na kasi ya kimaendeleo ya serikali ya awamu ya tano”alisema
Tweve
Tweve
alisema kuwa watendaji wanaohusika na sekta ya maji katika halmashauri
ya Mafinga Mjini wamekuwa hawafanyi kazi kwa weledi kwani tatizo
kuwabambikia bili wananchi limekuwa Sugu na kuongeza malalamiko mengi
huko mitaani hivyo lazima mbadilike maana swala la bili limekuwa kero
sana hapa Mafinga Mjini lazima mlitafutie ufumbuzi.
“Toka
nimerudi nimekuwa nikipokea malalamiko mengi yanayohusu bili za maji
naombeni tembeleeni nyumba kwa nyumba kuandika bili sahihi na sio kutoa
bili kwa kukisia hii inaalibu sura nzima ya viongozi wa halmashauri ya
Mafinga Mjini, narudia tena watendaji fanyeni kazi kwa kujituma acheni
mazoea kazini”alisema Tweve
Aidha
Tweve alimuomba Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanafanya
kazi za wananchi na sio kukaa tu ofisini kitu kinachosababisha
kuongezeka kwa matatizo kwa wananchi, hivyo mtalazimika kuwafuata
wananchi kujua changamoto zinazowakabili wananchi na kuzitafutia
ufumbuzi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga
alisema kuwa ahakikisha watendaji wote wanaenda kufanya kazi kwa
wananchi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kama ilivyokuwa miaka ya huko
nyuma na kuendelea kutekeleza Sera za chama cha mapinduzi CCM na
kuendena na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John
pombe Magufuli na kuwaletea maendeleo wananchi.
“Watendaji
wangu mmekisikia alichosema mbunge Rose Tweve kuhusu wajibu kwa kweli
hii ni aibu kubwa inatupaswa kujilekebisha ili kuendelea kutekeleza Sera
za serikali ya awamu ya tano la sivyo nitaanza kuwatumbua mmoja baada
ya mmoja ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa halmashauri ya
Mafinga Mjini”alisema Makoga
Lakini
Makoga aliwasifu wabunge Wawili ambao ni mbunge Cosato Chumi na Rose
Tweve kwa kufanya kazi kwa nguvu na kuleta maendeleo ya wananchi wa
wilaya ya Mufindi kwa ujumla maana kila siku tunapata mambo mapya ya
kimaendeleo kupitia migongo yao na kuwaomba waendelee kutafuta njia
nyingine za kuiletea maendeleo Mufindi.
“Miaka
yote tungekuwa na wabunge kama hawa wawili leo hii Mufindi ingekuwa
mbali sana kimaendeleo kutokana na Juhudi zao tunaziona maana saizi kila
secta wameigusa kwa kuleta maendeleo au mikakati ya kutatua changamoto
za maeneo husika” alisema Makoga
Nao
baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo wasema kuwa bado wazitafutia
ufumbuzi changamoto za Mji wa Mafinga licha ya kuwa na ufinyu wa bajeti
za kimaendeleo kwenye miradi waliyoiomba hivyo wakipewa bajeti na
kuajiri baadhi ya watumishi kila kitu kitaenda vizuri na changamoto za
wananchi zitatuliwa kwa wakati.

No comments :
Post a Comment