Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango
akisalimiana na wafanyakazi wa TPB Bank wakati alipowatembelea katika
banda la Wizara ya Fedha na Mipango, ambapo amewapongeza kwa kazi nzuri
wanayoifanya jambo ambalo limepelea kupata faida kutokana na huduma
zinazotolewa na benki hiyo, pia akuwapongeza kwa mara nyingine tena kwa
gawio walilotoa kwa serikali la bilioni 1 iliyopatikana katika faida ya
mwaka 2016.
Afisa Mawasiliano wa benki ya TPB Bank Bi. Chichi Banda
anawakaribisha wateja wote pamoja na wananchi wanaotembelea maonyesho
hayo watembelee banda lao lililopo kwenye jengo la wizara ya fedha na
mipango, TPB Bank itaendelea kuwepo kwenye maonyesho hayo hadi siku ya
mwisho ambayo ni tarehe 13
Picha mbalimbali zikionyesha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akipata maelezo mbalimbali wakati alipotembelea katika banda hilo.
No comments :
Post a Comment