Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la
Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza maandamano ya Mabalozi wa
Usalama Barabarani kuingia Uwanja wa Mashujaa, wakiadhimisha siku yao
iliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma leo.Kulia ni Katibu Mtendaji wa
baraza hilo,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed
Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la
Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa madereva kufuata
sheria ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo
zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga wa ajali
hizo.Wapili kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Mkuu wa Kikosi
cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga na anayefuatia ni
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa. Maadhimisho hayo
yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga, akizungumza wakati wa maadhimisho
ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa askari wa
usalama barabarani kusimamia sheria ili kuweza kupunguza tatizo la
ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi
kubwa ya wahanga wa ajali hizo.Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza
la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa
wa Dodoma,Lazaro Mambosasa. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja
wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa
Dodoma,Lazaro Mambosasa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya
Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwashukuru mabalozi hao kuchagua
mkoa wa Dodoma kufanyia maadhimisho hayo na kuahidi kuelimisha
watumiaji wa vyombo vya moto sheria na kanuni za usalama barabarani
ikiwa anaongoza mkoa ambao ni Makao Makuu ya nchi .Wakwanza kushoto ni
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia
ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia
ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed
Mpinga.Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo
mkoani Dodoma.
Mabalozi wa Usalama wa Barabarani
wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama
Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya
Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa madereva kufuata sheria
ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa
zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga wa ajali hizo.
Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani
Dodoma.
Msanii Faustine Matina ambae ni
Balozi wa Usalama Barabarani, akiimba wimbo wa kuhimiza masuala ya
kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wa Siku ya Maadhimisho ya
Mabalozi wa Usalama Barabarani, iliyofanyika kitaifa leo katika Uwanja
wa Mashujaa,mkoani Dodoma.
Mhanga wa ajali anayefahamika kwa
jina la Mpemba Asilia, akizungumza na Mabalozi wa Usalama Barabarani,
alipofika katikaMaadhimisho ya Mabalozi wa Usalama Barabarani
yaliyofanyika kitaifa leo katika Uwanja wa Mashujaa,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la
Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watano kulia),akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani yaliyofanyika
kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.Wasita kulia ni Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga
No comments :
Post a Comment