Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,
akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya nyumba za
watumishi (WHC) Dk. Fred Msemwa wakati alipotembelea banda la taasisi
hiyo leo kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya
Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke jijini Dar es salaam,
Katikati ni Afisa Masoko na Uhusiano wa (WHC)Bi. Maryjane Makawia.
Mara baada ya kutembelea banda
hilo Waziri Lukuvi amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali
haitaondoa (VAT) katika vifaa vya ujenzi hivyo taasisi mbalimbali
zinazojishughulisha na ujenzi wa nyumba zinatakiwa kujipanga na kuchukua
hatua mbalimbali za kupunguza gharama za ujenzi wa miradi yao ikiwa ni
pamoja na kutumia teknolojia rahisi na ya kisasa isiyochukua gharama
kubwa katika ujenzi wa nyumba.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiuliza swali kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi( WHC) Dk. Fred Msemwa katikati
wakati wakati alipotembelea katika banda hilo leo, kushoto ni Afisa
Mauzo (WHC) Bi. Irene Kasanda na wa pili kutoka kulia ni Afisa Masoko na
Uhusiano wa (WHC) Bi. Maryjane Makawia.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimsikiliza Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi (WHC) Dk. Fred Msemwa wakati
alipokuwa akifafanua mambo kadhaa kwa waziri alipotembelea katika
banda lao.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi (WHC) Dk. Fred Msemwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mh. Waziri William Lukuvi kuwatembelea katika banda lao kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa (WHC)Bi. Maryjane Makawia.
Afisa Mauzo (WHC) Bi. Irene Kasanda kushoto na Afisa Masoko na Uhusiano (WHC) Bi. Maryjane Makawia wakipozi kwa picha.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya nyumba za watumishi (WHC) Dk. Fred Msemwa akizungumza na mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda la taasisi hiyo.
No comments :
Post a Comment