Saturday, July 8, 2017

MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AIPONGEZA HATUA ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UWEKEZAJI KWENYE VIWANDA NA MPANGO WA WOTE SCHEME



 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kushoto), akitoa pongezi zake kwa PPF kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda ambapo Mfuko huo kwa ushirikiano na wabia wengine, umewekeza kwenye miradi mikubwa ya Mkulazi mkoani Morogoro na ule wa uboreshaji wa kiwanda cha viatu Karanga na ujenzi wa kiwanda kipya cha viatu kwenye eneo hilo kwa ubia na Magereza. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele akiwa na wafanyakazi wenzake.

(K-VIS BLOG/Khalfan Said)
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alitembelea banda hilo na kuipongeza PPF kwa uamuzi wake wa kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kujenga uchumi wa viwanda. Akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, alisema, utekelezaji wa miradi unaendelea vizuri kwa upande wa Mkulazi mkoani Morogoro na kiwanda cha viatu Karanga mjini Moshi ambacho kinaendeshwa kwa ubia na Jeshi la Magereza. Ukarabati wa kiwanda cha sasa unaendelea na unategemea baada ya kuweka mitambo mipya uzalishaji  utaongezeka kutoka jozi 150 za viatu hadi kufikia jozi 400 kwa siku, alisema Bi. Mengele. "Uboreshaji wa kiwanda hiki cha ngozi sio tu utaongeza uzalishaji bali pia tunakusudia kununua malighafi za ndani na pia tutakuwa tumeongeza ajira." Alifafanua Bi. Mengele.
Kwa upande wake, Waziri Dkt. Mpango ambaye alipata fursa ya kutembelea maeneo amabayo PPF imewekeza kwenye viwanda, alisema  "Ninyi ni watu wazuri na niwapongeze kwa uamuzi wenu mzuri wa kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano ambayo tumejikita katika kujenga uchumi wa viwanda " Alisema Dkt. Mpango.  Wakati huo huo Waziri Dkt. Philip Mpango, amewahimiza vijana kujiunga na PPF kupitia Mpango wake wa Wote Scheme, kwani kuna faida nyingi ambazo mwanachama aliyejiunga na Mpango huo atafaidika nazo. Dkt. Mpango alitoa rai hiyo wakati akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kupitia Mpango wa "Wote Scheme", kijana wa miaka 18, Msuya S. Mageta, kwenye banda la Mfuko huo.
Dkt. Mpango alifurahishwa na uamuzi wa kijana huyo na kuwataka vijana wengine kuiga mfano wake. Pia aliipongeza PPF kwa huduma zake za haraka baada ya kushuhudia mwanachama wa PPF akichangia michango kupitia simu yake ya kiganjani kwenye banda la Mfuko huo. Waziri alitoa rai kwa wananchi kujiunga na Mfuko huo kwani umepata mafanikio makubwa kwa kuweza kupata cheti cha ubora wa kimataifa kwa kutoa huduma bora zenye kiwango cha kimataifa (ISO 9001;2015) ambapo ndio Mfuko pekee wa Hifadhi ya Jamii kupata hati hiyo.
 Waziri Dkt. Mpango, akimpongeza Bw.Sukulu Mageta, ambaye ni mzazi wa Msuya Mageta, (katikati), kijana wa miaka 18 aliyeamua kwa hiari yake kujiunga na mpango wa Wote Scheme.
 Meneja Elimu kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi mkoba wenye vipeperushi vya taarifa za PPF, Waziri Dkt. Mpango.
 Bi. Lulu Mengele akitoa maelezo mbele ya Dkt. Mpango kuhusu huduma zitolewazo na PPF
 Dkt. Mpango akisikiliza kwa makini maelezo ya Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele
 Bi. Lulu Mengele akitoa maelezo mbele ya Dkt. Mpango kuhusu huduma zitolewazo na PPF
 Bw.Sukulu Mageta, mzazi wa Msuya Mageta, akieleza ni kwa nini aliamua kumuunga mkono kijana wake Msuya, kujiunga na PPF. Alisema, "Mimi kama mzazi uamuzi wa kijana wangu kujiunga na PPF, ni uamuzi sahihi na hii itanirahisishia hapo baadaye ambapo kwa mujibu wa maelezo tuliyopewa na maafisa wa PPF, mwanachama anaweza kupata mafao mbalimbali yakiwemo ya kujiendeleza kielimu, lakini pia bima ya afya na kijana wangu ndio kamaliza kidato cha sita na anahitaji kuendelea na masomo, kwa hiyo baadaye atafaidika ikiwa ni pamoja na kujiwekea akiba". Alisema Bw. Mageta
Waziri Dkt. Mpango, akishuhudia jinsi, Bw Edwin Makamba, (wapili kulia), ambaye ni mwanachama wa PPF kupitia mpango wa Wote Scheme, akichangia kupitia simu yake ya mkononi. wengine pichani ni Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (kulia) na Meneja Elimu kwa Wanachama wa Mfuko huo, Bw. Kwame Temu. (kushoto).
Waziri Dkt. Philip Mpango, akikaribishwa kwenye banda la Wizara ya Fedha na Mipango, na Mkuu wa Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,(kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kupitia Mpango wa "Wote Scheme", kijana wa miaka 18, Msuya S. Mageta, kwenye banda la Mfuko huo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasaba ambako kunafanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam. Waziri Mpango leo Julai 8, 2017.
 Mpango wa Wote Scheme, umebuniwa na Mfuko huo ili kutoa fursa kwa watu wa makundi mbalimbali kama vile mama lishe , wakulima, machinga, waendesha bodaboda na mtu yeyote mwenye kufanya kazi halali yenye kumpatia kipato kuwa mwanachama.

No comments :

Post a Comment