Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akisalimiana na mama Zakia Megji wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu
Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia
Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli,
(kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani Julai 9,
2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani wakati wa
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu
mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais
Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema
Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akipokea shada la maua wakati akikaribishwa kwenye maadhimisho ya miaka
60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya
Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli,
(katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akisaini kitabu cha wageni kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu
Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia
duniani, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani na
(kulia) ni muwakilishi wa AKDN Resident Amin Kurji, wakati
alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya
Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akizungumza na Muwakilishi wa AKD resident Amin Kurji katika maadhimisho
ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa
madhehebu ya Shia Ismailia duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa
Diamond Jubilee, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli,(katikati)
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan Suleiman Shabbudin
Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akiteta jambo na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani, katika
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu
mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais
Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akipokea maandano ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo
chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee, Waziri Mkuu
amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika sherehe hiyo, Julai 9,
2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
*Asema nchi ina utulivu wa kisiasa na uchumi unaokuwa kwa kasi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji
watakaokuja nchini kwa
kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye
kukua kwa kasi.
Ameyasema hayo leo (Jumapili,
Julai 09, 2017) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu
Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.
Waziri Mkuu amesema Serikali
inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa
taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea
kushirikiana nao.
Ameupongeza mtandao wa taasisi za
Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele
cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji
ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Nawahakikishia kwamba uwekezaji
wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi imetulia kisiasa na
uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa
madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini
fursa bado zipo.”
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya
ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw. Amin Lakhani ameishukuru
Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea
kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali nchini.
Amesema mtandao wa maendeleo wa
Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya, elimu, kilimo na
kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa fursa watu
wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua
kiuchumi.
Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilala,
Bi. Sophia Mjema aliipongeza taasisi hiyo kwa mpango wake wa upanuzi wa
hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka 15 walivyonavyo.
No comments :
Post a Comment