Dkt. Philip Mpango-Waziri wa Fedha na Mipango akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa TRA wakati alipotembelea katika banda la wizara yake.
……………………………………………………………
BENNY MWAIPAJA, WFM, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, amewapongeza Watanzania nchini kote kwa mwitikio wao
mkubwa wa kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ya majengo kwa hiari, hatua
ambayo itaiongezea Serikali uwezo wa kuwahudumia kupitia utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo
alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
katika uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwal. J. K. Nyerere, Barabara
ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Ametoa wito kwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania TRA kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa
kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa pamoja na kuwahimiza wananchi kudai
risiti wanapofanya manunuzi halkadhalika wafanyabiashara kutoa risiti
wanapouza bidhaa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Baadhi ya wananchi waliofurika
kulipa kodi mbalimbali hususan za majengo katika viwanja hivyo vya
Sabasaba, wameeleza kuwa mwitikio na hamasa kubwa waliyonayo ya kulipa
kodi inatokana na imani yao kwa Serikali ya Awamu ya Tano jinsi
inavyosimamia maendeleo ya nchi kwa umakini mkubwa.
Kwa upande wake Meneja wa Huduma
kwa Mlipakodi Bi. Honesta Nduguru, amewataka Watanzania popote walipo
kutumia muda mfupi wa nyongeza uliobaki kulipa kodi badala ya kusubiri
dakika za lala salama.
No comments :
Post a Comment