Afisa Mwandamizi wa Idara ya
Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adam Msumule akitoa elimu ya
Bajeti kwa wananchi waliotembelea katika banda la Wizara hiyo katika
maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipeana mkono na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, walipokutana katika viwanja vya Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kulia) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa Shirika
la Bima la Taifa (NIC) kuhusu namna ya kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa
umma kuhusu umuhimu wa kukata bima ili kujikinga na majanga,
alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango lilipo katika viwanja
vya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Sam Kamanga.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi
wa uendeshaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Naftal
Sigwejo baada ya kuulizwa kuhusu ubora wa baadhi ya bidhaa zinazotolewa
Serikalini baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango
katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipata maelezo kutoka Mfuko wa
Pensheni wa GEPF kuhusu huduma na mchango wa mfuko huo katika maendeleo
ya viwanda, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya
Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipata maelezo kutoka Banda la
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu njia ya kisasa ya ufugaji Samaki
alipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akimpongeza mtumishi wa Suma JKT
baada ya kutoa maelezo ya mtambo wa kuvuta maji katika viwanja vya
maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
No comments :
Post a Comment