Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la
kutoa huduma za Elimu ya afya Nchini Marekani Bi. Asha Mustafa
Nyang’anyi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu ujio wao hapa
Zanzibar.
Bwana. Amiri Muhammed Amiri
akimuonesha fangas Daktari bingwa wa ngozi Mamotheo alipokuwa akitoa
matibabu katika hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Baba wa mtoto Abdulmajid
akiwaonesha madaktari bingwa wa maradhi ya ngozi namna mwanawe
alivyodhurika kwa kufanya mabaka mwilini katika hospitali ya Mnazimmoja
mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.
…………………
Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar
Wananchi wa Tanzania wanaoishi
Marekani wanadiaspora wakishirikiana na
Madaktari bingwa wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua wananchi.
Madaktari bingwa wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua wananchi.
Zoezi la kutoa huduma hizo za matibabu bure linafanyika kwa muda wa siku tatu katika Hospitali ya Mnazi mmoja.
Akizungumza na waandishi wa
habari huko katika kitengo cha maradhi ya ngozi kwenye hospitali kuu ya
Mnazi mmoja, Mwanadiaspora Idi Seif Sandaly amesema wameamua kuja
nchini hapa kutoa huduma hizo ili kuwasaidia wananchi wenye matatizo
mbalimbali.
“Tumekuja Zanzibar kwa lengo la
kuwasaidia wananchi ambao wana maradhi mbali mbali na kuwapatia matibabu
kwa kupitia jumuiya yetu ya marekani Health Education Development kwa
kutibu maradhi ya ngozi , sukari na pressure pamoja na maradhi ya
akinamama.” Amesema Mwanadiaspora huyo.
Sandaly amesema wapo kwa muda wa
siku tatu na wamekuja na dawa za kutibia maradhi hayo ambapo dawa hizo
wanazitoa bure bila ya gharama zozote kwa wananchi.
Amesema katika matibabu yao
wanatarajia kutoa huduma kwa zaidi ya Wananchi 3,000 watakaofika katika
Hospital hiyo ya Mnazi mmoja.
Akifafanua kuhusu gharama za Dawa
hizo ambazo wamekuja nazo kutoka Marekani amesema zaidi ya Dola Million
moja za Marekeni zimetumika kwa ajili ya kununulia Dawa hizo.
Hata hivyo ameongeza kuwa Nusu za
Dawa hizo zitatumika Zanzibar na Nusu yake zitapelekwa Mkoa wa Bukoba
kwa lengo la kusaidia matibabu mkoani huko
Nae Daktari wa maradhi ya Ngozi
kutoka Marekeni Dkt Mamotheo Lepheana amesema amefarijika kuona wananchi
wamejitokeza kwa wingi hasa wa maradhi ya ngozi.
Sambamba na hayo mgonjwa
aliyepata matibabu hayo ya ngozi Masika Juma Mussa mkaazi wa Mwera
amesema ameshukuru kupatiwa huduma hiyo na kuiomba serikali iendeleze
kuleta wataalam kama hao wanaotaka kusaidia jamii .
Kwa upande wake Mkurugenzi
mtendaji wa Shirika hilo la kutoa huduma za Elimu ya afya Asha Mustafa
Nyang’anyi amesema ameamua kuja Zanzibar kwa sababu wananchi wa hapa ni
wakarimu na wanaojali kusaidiwa.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments :
Post a Comment