Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi William Tate Ole Nasha akizungumza wakati wa siku ya Korosho
iliyofanyika leo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es
Salaam. Siku hiyo imewekwa maalum ili kuwahamasisha wananchi kutumia zao
la Korosho kama chakula ili kuwanufaisha kiafya na kiuchumi.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Korosho Tanzania Mhe. Edgar Mahokola Majogo akizungumza wakati wa siku
ya Korosho iliyofanyika leo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya
Biashara Dar es Salaam. Siku hiyo imewekwa maalum ili kuwahamasisha
wananchi kutumia zao la Korosho kama chakula ili kuwanufaisha kiafya na
kiuchumi.
Wananchi wakiwa katika
pilikapilika katika maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es
Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaa leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Tantrade Edwin Rutegaruka (mstari wa mbele wa pili kushoto) akifuatilia
uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kula Korosho
iliyofanyika leo katika maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es
Salaam.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Tate Ole Nasha, Katibu Mkuu wa Wizara ya
hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho
Tanzania Bw. Hassan B. Mkali wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya
uhamasishaji wa wananchi kula Korosho iliyofanyika leo katika maonesho
ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi William Tate Ole Nasha akigawa Korosho kwa baadhi ya wananchi
wakati wa siku ya Korosho iliyofanyika leo katika Maonesho ya 41 ya
Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam. Siku hiyo imewekwa maalum ili
kuwahamasisha wananchi kujenga utanaduni wa kula Korosho kama chakula
ili kuwanufaisha kiafya na kiuchumi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, William Tate Ole Nasha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
(Idara Kuu ya Kilimo) Mhandisi Edwin Mtigumwe na Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya Korosho Tanzania Edgar Mahokola Majogo wakionyesha pakiti za
Korosho mara baada ya kuzindua rasmi Kampeni ya kuhamasisha wananchi
kula Korosho leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
………………………………
Frank Mvungi-Maelezo
Wakulima wa Korosho nchini
wamejipatia zaidi ya shilingi bilioni 800 kutokana na...
mauzo nje ya nchi
katika msimu uliopita wa mauzo zao hilo.
Takwimu hizo zimetolewa leo na
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate ole Nasha
wakati akifungua madhimisho ya siku ya Korosho iliyoadhimishwa kama
sehemu ya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam
(Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere,
Barabara ya Kilwa.
“Serikali imekuja na utaratibu wa
kuagiza mbolea kwa mkupuo na pia tutaanza kutoa mbolea kwa bei elekezi.
Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tunawainua
wakulima wa Korosho na sekta ya kilimo kwa ujumla”, Aaisisitiza Ole
Nasha.
Aliongeza kuwa tani elfu 18 za
mbolea aina ya salfa zitatolewa kwa wakulima bila malipo katika msimu
ujao wa korosho hali itakayosaidia kuwaongezea ari wakulima wa korosho
ambalo ndilo zao lililoingizia Taifa fedha nyingi zaidi za kigeni msimu
uliopita.
Katika kuwawekea wakulima
mazingira wezeshi Mhe. Ole Nasha alisema Serikali imeondoa tozo zaidi ya
140 zilizokuwa kero kwa wakulima hapa nchini ikiwa ni sehemu ya
mikakati ya kukuza kilimo kwa maendeleo ya viwanda na uzalishaji wa
ajira.
“Kukua kwa kilimo kutasaidia
kuongeza ajira kwa vijana wetu wanaohitimu masomo katika vyuo mbalimbali
ndio maana tunaweka mkazo katika kukuza zao hili ambalo lina faida si
za kibiashara tu bali pia katika kujenga afya ikiwemo kupunguza lehemu
mwilini, uzito na kujenga kinga ya mwili”, alisisitiza Ole Nasha.
Kwa kuzingatia umuhimu huo alitoa
wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kula korosho kwani kwa kufanya
hivyo watakuwa wanakuza soko la ndani.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Kilimo) Mhandisi Methew Mtigumwe amesema
siku ya Korosho katika maonesho ya Sabasaba ni muhimu kwa kuwa
inawakutanisha wadau wa sekta hiyo kwa pamoja.
Pia aliwapongeza wananchi kwa
kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho hayo hali inayoonyesha kuwa
sasa kuna mageuzi makubwa katika sekta hiyo.
Bei ya Korosho katika msimu
uliopita kwa Kilogramu moja iliuzwa shilingi 4000/- hali inayoonesha
kuwa wananchi wakiunga mkono juhudi za Serikali kwa kuzalisha kwa wingi
na kuongeza thamani ya korosho wanazozalisha basi zao hilo linaweza
kutoa mchango mkubwa zaidi katika kujenga uchumi wa viwanda.
No comments :
Post a Comment