Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo, wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa bei za dawa, vifaa, vifaa
tiba na vitendanishi vya maabara kutokana na uamuzi wa serikali wa
kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu
wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Viongozi
wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Elangwa, Mkurugenzi Mkuu
MSD, Laurian Bwanakunu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Kaimu Mfamasia
Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya, Siana Mapunjo na Mfamasia
kutoka Wizara hiyo, Mercy Masuki.
Taarifa ikitolewa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanahabari Ibrahim Yamola akiuliza swali.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanahabari, Philip David akiuliza swali.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
amesema bei za dawa, vifaa tiba na Vitendanishi vya maabara
zinazonunuliwa na... kusambazwa Boahari ya Dawa (MSD) zimepungua bei kwa
asilimia 15 hadi 80 ukulinganisha na mwaka jana kutokana na hatua ya MSD
kuanza utaratibu wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kama
alivyo agiza Rais Dk.John Magufuli.
Waziri
huyo ameyasema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari,
alioufanya ofisi za Makao Makuu ya Bohari ya Dawa MSD, Keko, Dar es
Salaam leo huku akizielekeza Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya
kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa ma Wizara ya Afya ambayo ipo
kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.
MSD
kwasasa inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji
wanchizipatazo 20 ambazonipamojana Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India,
Bangladesh, Pakistan, Jamuhuri ya Watu wa Korea, China, Ujerumani,
Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji, Italia, Romania,
Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu, na Tanzania.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema
tayari wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya hiyo 46 ni ya
wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark, Ufaransa,
Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu,Bangladesh,
India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.
Baadhi
ya dawa hizo ni pamoja na dawa ya chanjo ya homa ya ini (hepatitis B
Vaccine ) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 22,000 sasa inauzwa shilingi
5,300, Dawa ya sindano ya Diclofenac kwa ajili ya maumivu (vichupa 10)
awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 2,000 sasa inauzwa shilingi 800 na Dawa
ya kupambana na maambukizi ya bacteria (Amoxicillin/Clavulanic Acid
Potassium 625mg) yenye Vidonge 15 awali iliuzwa shilingi 9,800 sasa
inauzwa shilingi 4,000.
Kwa
upande wa vifaa tiba amesema jumla ya wazalishaji 18 wamepata mikataba
ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na Tanzania, kwa ajili
ya aina 195 za vifaa tiba.Aidha, kwa upande wa vitendanishi vya
maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za Uingereza, Ujerumani,
Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata mikataba kwa ajili ya
aina 178 za vitendanishi vya maabara.
Kwa
mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto,Serikali ya awamu ya tano imeboresha kwa kiasi kikubwa hali ya
upatikanaji wa dawa nchini ambapo bajeti ya dawa,vifaa tiba,
vitendanishi vya maabara na chanjo kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni
shilingi Bilioni 269 kutoka Bilioni 251 ya mwaka jana wa fedha
92016/2017)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments :
Post a Comment