Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto), akikagua ujenzi
wa Nyumba za viongozi zinazojengwa na Wakala Wa Majengo nchini (TBA)
Mkoani Katavi, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bi. Rachel
Kassanda.
Meneja Wa Wakala Wa Barabara
nchini (TANROADS), Eng. Abdon Maregesi (kulia), akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani
(Katikati) juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Kivuu wakati
Naibu Waziri huyo alipokagua, Mkoani Katavi.
Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wananchi wa kata ya
MajiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi mara baada ya kukagua Daraja la
Kavuu ambalo ujenzi wake umekamilika na linatarajiwa kuanza kutumika
mwishoni mwa mwezi huu..
Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akisalimiana na wakazi wa kata ya
MajiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi mara baada ya kuongea nao.
Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akiongea na Mbunge wa Jimbo
la Manyoni Magharibi Mhe. Omary Yahya Massare (Kulia), Wakati Waziri
Ngonyani alipotembelea Jimboni kwake mwishoni mwa wiki.
Muonekano wa Daraja la Kavuu lenye
urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ambalo ujenzi wake
umekamilika kwa asilimia 99.
Muonekano wa Barabara ya
Sitalike-Mpanda yenye urefu wa kilomita 36.9 ambapo ujenzi wake
umekamilika kwa asilimia 99, barabara hii ni sehemu ya barabara kuu
inayoanzia Tunduma kupitia Sumbawanga, Mpanda, Uvinza, Kibondo,
Nyakanazazi hadi Mutukula.
…………………….
Ujenzi wa Daraja la Kavuu lenye
urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya...
Mlele na
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ujenzi wake umekamilika
na litaanza kutumika ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kukagua
ujenzi wa Daraja hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha
usafirishaji wa abiria na Mizigo kutoka Mkoa wa katavi kwenda mikoa ya
jirani.
“Serikali iliona kero kubwa
wanazozipata wananchi wa mkoa huu hasa kwenye usafirishaji wa abiria na
mizigo kwenye kipindi cha mavuno, hivyo baada ya kukamilisha Daraja hili
wananchi wataweza kupita vipindi vyote vya Mwaka,” alisema Naibu Waziri
Eng. Ngonyani.
Aidha, Eng. Ngonyani amemuagiza
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Katavi Eng. Abdon
Maregesi Kuhakikisha Mzani unaohamishika unawekwa ili kudhibiti magari
yatakayozidisha Tani 36.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala
wa Barabara Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi amemuhakikisha Naibu
Waziri, Eng. Ngonyani kuwa wakala utaweka mzani huo ili kutoruhusu
magari yaliyozidisha Uzito wa Mzigo kupita kwenye Daraja hilo.
Wakati huo huo, Naibu Waziri Eng.
Ngonyani amekagua ujenzi wa Nyumba za Viongozi Mkoani humo na kuuagiza
Wakala wa Majengo nchini (TBA), kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo
unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.
“Serikali imeshatoa fedha za
kukamilisha ujenzi wa nyumba hizi, ujenzi huu ulisimama kwa takribani
miezi minne kwa sasa hakuna sababu ya ujenzi kusuasua wakati fedha zipo,
ninakuhakikishia Mkuu wa Wilaya nyumba hizi zitakamilika kwa wakati ili
zianze kutumika,” alisisitiza Naibu Waziri Eng. Ngonyani.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri
Eng. Nyonyani amekagua ujenzi wa Barabara ya Sitalike-Mpanda yenye
urefu wa kilomita 36.9 ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99,
barabara hii ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Tunduma kupitia
Sumbawanga, Mpanda, Uvinza, Kibondo, Nyakanazazi hadi Mutukula.
Naibu Waziri Eng. Ngonyani yupo
katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya Ndege,
Ujenzi wa Nyumba za viongozi na Madaraja katika Mkoa wa Katavi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment