Mkurugenzi wa Utawala na Fedha
kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (kulia) akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Kagera. Kushoto ni Meneja Mipango
Miradi na Tafiti kutoka wakala huo, Mhandisi Jones Olotu
Meneja wa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze akifafanua
jambo kwa timu ya maandalizi ya uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa
Umeme Umeme Vijijini Awamu yaTatu (REA III) katika mikoa ya Kagera,
Geita, Mwanza na Simiyu (hawapo pichani)
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha
kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (kulia)
akielezea mikakati ya usambazaji wa umeme vijijini nchini kwa Meneja wa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis
Maze (hayupo pichani) katika ofisi za TANESCO mkoani Kagera. Kushoto ni
Meneja Mipango Miradi na Tafiti kutoka wakala huo, Mhandisi Jones
Olotu.
Mkurugenzi Msaidizi (Uzalishaji)
kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Abdallah Ikwasa
(kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko
na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi
Elineema Mkumbo (kulia) katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) mkoani Kagera.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera
Diwani Athuman (mbele) akizungumza na timu ya watendaji kutoka Wakala
wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na
wakandarasi ofisini kwake kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali
Mstaafu, Shaban Lissu (katikati) akisalimiana na Mkurugenzi wa
Uendelezaji wa Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini
(REA), Elineema Mkumbo (kulia) mara baada ya timu ya maandalizi
kuwasili katika eneo la Rwabigaga wilayani Kyerwa ambapo kutafanyika
uzinduzi huo kwa mkoa wa Kagera
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha
kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (wa pili kulia)
akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali Mstaafu, Shaban
Lissu (kushoto) katika eneo la Rwabigaga wilayani Kyerwa ambapo
kutafanyika uzinduzi huo kwa mkoa wa Kagera
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali Mstaafu, Shaban Lissu (kushoto) akifafanua jambo
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha
kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (kushoto)
akielezea miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala huo. Kulia
ni Meneja Mipango Miradi na Tafiti kutoka wakala huo, Mhandisi Jones
Olotu.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha
kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (wa pili
kushoto) akitoa maelekezo kwenye eneo la jiwe la msingi kwa ajili ya
uzinduzi wa Mradi wa REA Awamu ya Tatu ambalo liko katika hatua za
mwisho wa ukamilishwaji wake.
No comments :
Post a Comment