Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni
katika banda la Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji alipotembelea
Maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba)
yanayofanyika katika Viwanja vya J.K. Nyerere barabara ya Kilwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akitazama bidhaa
zinazozalishwa ndani ya nchi katika moja ya banda alipotembelea Maonesho
ya Kimataifa ya 41 ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika
katika Viwanja vya J.K. Nyerere barabara ya Kilwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akitazama samani
zinazotengenezwa ndani ya nchi katika banda la Kampuni ya WOISO Product
alipotembelea Maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara Dar es Salaam
(Sabasaba) yanayofanyika katika Viwanja vya J.K. Nyerere barabara ya
Kilwa. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tantrade Mhandisi
Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kutoka
kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Abdul Haleem Zahran kuhusu
bidhaa za ujenzi zinazotengenezwa hapa nchini alipotembelea banda la
Kampuni ya Property International katika Maonesho ya Kimataifa ya 41 ya
Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Tantrade Mhandisi Christopher Chiza.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Peter
Pinda akifafanua jambo alipotembelea banda la Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA) katika maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara Dar es Salaam
(DITF) leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji (Idara Kuu ya Biashara), Profesa Aldof Mkenda.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo
Peter Pinda akifuatilia maelezo kutoka kwa mmoja wa waonyeshaji katika
eneo la bustani ya mahindi ya Kampuni ya uzalishaji wa mbegu ya Seed Co
katika maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
……………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka Taasisi za fedha
kuwawezesha wajasiriamali ili waweze kushiriki katika ujenzi wa...
uchumi
wa viwanda.
Akizungumza mara baada ya
kutembelea maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Dar es Salaam (Sabasaba) Mama
Samia taasisi za fedha zinaowajibu wa kuwawezesha wajasiriamali ili
wapate mitaji ya kuendeleza biashara zao.
“Serikali itaendelea kuhamasisha
taasisi za fedha hapa nchini ili ziendelee kuwawezesha wajasiriamali na
hatimaye kwa pamoja tufikie azma ya Tanzania ya Viwanda.”alisema Mama
Samia.
Aidha Mhe. Samia alisema kuwa
Maonesho ya mwaka huu yamezidi kuongeza ubunifu kutokana na kuongezeka
kwa ubora wa bidhaa za ndani ya nchi.
“Kwa ujumla niseme tu maonesho ni
mazuri na tumeongeza muda ili watanzania wengi zaidi waje watembelee na
kujionea bidhaa mbalimbali na huduma zinazotolewa “ Alisisitiza Mhe.
Samia
Akifafanua amesema kuwa kuna
mabadiliko makubwa hasa katika mabanda ya kina mama kwa kuwa bidhaa
wanazozalisha zina ubora unaoendana na mahitaji ya soko.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa Serikali
imejipanga kuhakikisha kuwa viwanda vyote walivyopewa wawekezaji
vinaendelezwa na kuzalisha kwa tija.
Aliongeza kuwa Viwanda vya
kuzalisha bidhaa za ngozi kama kile cha BORA sasa vimeanza uzalishaji
kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali yaliyowataka wale wote waliopewa
viwanda na Serikali kuviendeleza ili vitoe matokeo kusudiwa.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi
ya Tantrade Mhandisi Christopher Chiza ametoa wito kwa wakazi wa Dar es
Salaam kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ambapo kesho ni siku ya
sikukuu ya sabasaba.
Maonesho haya ya Kimataifa ya 41
ya Biashara Dar es Salaam (DITF) yalianza Juni 28 na yanatarajiwa
kumalizika Julai 13 ambapo yanashirikisha takribani nchi 30 na Makampuni
zaidi ya 2500 huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Ukuzaji wa Biashara kwa
Maendeleo ya Viwanda”.
No comments :
Post a Comment