Friday, July 7, 2017

ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI AAGWA DAR

unnamed
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro, wakati akiwasili kwenye msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, (katikati) ni Katibu Mkuu Ikulu Alphayo Kidata, Julai 7, 2017.
1Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
2
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akishiriki dua ya kumuombea marehemu ya aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
3
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, akisaini kitabu cha maombolezo, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017
4
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitoa pole kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, viongozi waandamizi wa Serikali na mamia ya wananchi kuuaga mwili wa ...
aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Bw. Hassan Shebuge.
Marehemu Bw. Shebuge ameagwa leo (Ijumaa, Julai 7,2017) nyumbani kwake Mbagala- Majimatitu jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Julai 8, 2017), katika kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
Bw. Shebuge amefariki dunia jana (Alhamisi, Julai 6, 2017) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata na shinikizo la damu.
Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali.
Amesema enzi za uhai wake marehemu Bw. Shebuge alikuwa mpole na muadilifu na kutoa  mchango mkubwa kwenye kufanikisha maamuzi na utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa ufanisi.
“Kwa kweli hatuna budi kwa sasa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.”
Awali, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata akisoma wasifu wa marehemu Bw. Shebuge alisema marehemu alizaliwa Mei 25, 1969 wilayani Korogwe, Tanga.
Alisema marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya Mkwakwani kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1983, ambapo alipata elimu ya sekondari katika shule ya Usagara kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, zote za mkoani Tanga.
Bw. Kidata alisema mwaka 1988, marehemu alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mkoani Arusha kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na cha sita.
Alisema mwaka 1992 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya Sanaa na Ustawi wa Jamii mwaka 1995, mwaka 1998 alipata shahada ya uzamili ya Sanaa na Ustawi wa jamii. Pia marehemu alipata mafunzo mengine mbalimbali ndani na nje ya nchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JULAI 07, 2017

TANZIA: KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI, HASSAN SHEBUGE AFARIKI DUNIA

Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge (pichani) kilichotokea Julai 06, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbini Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Kabla ya kufikwa na Mauti, inaelezwa kuwa Marehemu Shebuge aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake, Mbagara Majimatutu mnamo Julai 03, 2017 na kukimbizwa katika Hospitali ya Rangi tatu ili kupatiwa huduma ya dharula na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbini kwa matibabu zaidi hadi hapo matuti yalipomfika.
Kwa mujibu wa taarifa ya kitaama iliyotolewa na madaktari, inaelezwa kuwa Maremu Shebuge alipatwa na shinikizo la damu ambalo limepeleka kupoteza kwake maisha.
Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu, aiweke roho ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge mahapa pema peponi, Amin.
Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu.
IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA 



Katika picha hii ya maktaba, Karani wa Baraza la Mawaziri, Bw. Hasan Ramadhan, (wapili kulia), akishuhudia wakati Rais John Pombe Magufuli akimuapisha mmoja wa mabalozi hivi karibuni, Ikulu jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAMIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Baba Mdogo wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge, Bw. Juma Hassan Shebuge mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mbagala Rangi Tatu.
Marehemu Hassan Shebuge ambaye alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri alifariki jana tarehe 6, Julai katika hospitali ya Muhimbili kwa shinikizo la Damu.
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge,nyumbani kwa marehemu Mbagala Rangi Tatu.
Marehemu Hassan Shebuge ambaye alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri alifariki jana tarehe 6, Julai katika hospitali ya Muhimbili kwa shinikizo la Damu
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole na kumfariji mjane wa  Marehemu Hassan Rashid Shebuge,nyumbani kwa marehemu Mbagala Rangi Tatu.
Marehemu Hassan Shebuge ambaye alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri alifariki jana tarehe 6, Julai katika hospitali ya Muhimbili kwa shinikizo la Damu.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili  Marehemu Hassan Rashid Shebuge,nyumbani kwa marehemu Mbagala Rangi Tatu.
Marehemu Hassan Shebuge ambaye alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri alifariki jana tarehe 6, Julai katika hospitali ya Muhimbili kwa shinikizo la Damu.
4
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa salaam za Serikali mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Hassan Rashid Shebuge.
Marehemu Hassan Shebuge ambaye alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri alifariki jana tarehe 6, Julai katika hospitali ya Muhimbili kwa shinikizo la Damu. (# Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments :

Post a Comment