Sunday, July 2, 2017

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA TANTRADE VIWANJA VYA SABASABA

n1
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bwana Sam Kamanga akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo  wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya 41 ya  Biashara  yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam maonyesho hayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE na kufanyika kila mwaka mwezi julai.
n2 n3
Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Elisante Maleko wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maonyesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
n4
Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maonyesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Elisante Maleko 
ni4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la shirika la Bima la Taifa NIC Kulia ni Afisa Mwandamizi wa Bima Bw. Jumanne Nyamgunda.

No comments :

Post a Comment