Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
uhuru Amour Hamad Amour akifungua maji katika bomba wakati wa uzinduzi
wa mradi huo katika kijiji cha Merya Wilayani Singida, pembeni yake
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Fredrick Ndahani.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
uhuru Amour Hamad Amour akimtwisha ndoo ya maji moja ya akina mama
waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha
Merya Wilayani Singida.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
uhuru Amour Hamad Amour akitazama vitunguu katika shamba la mboga mboga
la umwagiliaji kwa njia ya matone wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika
kijiji cha Msange Wilayani Singida.
Sehemu ya shamba la mbogamboga
lenye kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone ambapo vitunguu
vinaonekana vimestawi vizuri, shamba hilo lina ukubwa wa ekari 25.
…………………….
Wanawake wa Vijiji vya Merya na
Ikugha katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida wameushukuru Mwenge wa
Uhuru kwa kuwafungulia mradi ambao umewaepusha kutembea umbali mrefu
kutafuta maji ya kutumia ambayo si safi wala salama huku wakiyachangia
na
mifugo yao.
Wanawake hao wametoa pongezi hizo
mara baada ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour
kufungua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 49
utakaohudumia vijiji hivyo ambao umegharimiwa na shirika la saving
International, halmashauri ya Singida pamoja na michango ya wananchi.
Wamesema kabla ya kupatikana mradi
huo wanawake wa vijiji hivyo wamekuwa wakifuata maji umbali mrefu sana
kiasi cha kushindwa kutekeleza shughuli nyingine za kuzalisha mali.
“Tulikua tunatembea mpaka
tunachoka, tunaamua kupumzika njiani kwanza ndio tuendelee na safari ya
kuleta maji nyumbani, yani tunashukuru sana kwakweli”, ameongea Bi Greta
Senge Mkazi wa kijiji cha Ikugha.
Aidha wameongeza kuwa mradi huo
utawapatia maji safi na salama kwakuwa maji waliyokuwa wakiyafuata
umbali mrefu hapo awali yalikuwa machafu na si salama.
“Yani tulikuwa tunachota maji
ambayo unakuta ng’ombe anakunywa hapohapo, wakati mwingine anajisaidia
na inabidi uchote hivyo hivyo, kwakweli tunaushukuru sana mwenge
kutufungulia mradi huu, tulikua tunaumwa matumbo kila mara”, ameongeza
Rehema Lazaro.
Wameongeza kuwa mradi huo
utapunguza magonjwa ya tumbo na macho ambayo yamekuwa yakiwasumbua mara
kwa mara hukua wakiridhia kulipia kiasi cha shilingi 50 kwa lita 20 za
maji ili kupata fedha za kutunza mradi huo.
Kwa upande wake kiongozi wa Mbio
za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour ameitaka jumuiya ya watumia maji ya
mradi huo kuutunza mradi huo ili utoe maji kwa wingi na muda huo
kutokanana kuonekana ni hitaji la muhimu.
“Nimefika hapa na kushuhudia akina
mama wengi mnamiminika na ndoo ili mpate maji, hii ni ishara kuwa mradi
huu ni muhimu hivyo basi jumuiya ya watumia maji hakikisheni mda wote
maji yanatoka na sio kupanga masaa ya kutoa maji au mvua ikinyesha tu
mnayafunga, hapana” amesisitiza Amour.
Amesema mradi huo usimamiwe vizuri
kusiwe na upendeleo au ubaguzi wowote kwakuwa maendeleo hayo hayana
ubaguzi wa rangi, dini, itikadi za kichama au makabila.
Amour amesema jumuiya hiyo
ihakikishe miundombinu ya mradi huo inatunzwa ili kuepusha kuwarudisha
akina mama hao katika shida waliyokuwa wakiipata awali huku akiwashauri
kuangalia namna ya kuipatia mifugo maji pamoja na kuweka taratibu nzuri
za mapato na matumizi ya mradi huo.
Wakati huo huo Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru amezindua mradi wa umwagiliaji mbogamboga kwa njia
matone wa ekari 25 wenye thamani ya shilingi milioni 326 katika kijiji
cha Msange.
Akisoma taarifa ya mradi huo Afisa
Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Adam Mngale amesema mradi
huo ulianzishwa mwaka 2012 na hadi sasa una wanachama 32 ambao
wananufaika kwa kujiongezea kipato kutokana na kulima misimu miwili yani
kiangazi na masika.
Mngale amesema malengo ya mradi
huo ni kuongeza eneo la uzalishaji hadi kufikia ekari 1400, kupanua
miundombinu ili waweze kutumia kutumia bwawa la suke na lililoko eneo
jirani katika umwagiliaji na kutumia kiwanda cha kusindika mbogamboga
kilichoko Msange kusindika mazao yao.
No comments :
Post a Comment