Wanafunzi UDSM wakisikiza kwa makini manufaa ya kujiunga na program ya Global Management Training ya ABInBev
meneja
vipaji wa kampuni ya ABInBev Afrika ,Cindy Rautenrouch,akielezea
mikakati ya kampuni hiyo kuandaa viongozi wa baadaye wa kuendesha
shughuli za kampuni
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Emmanuel Mwanuke akimuuliza swali Meneja Mikakati wa TBL Group,Magabe Maasa (kulia)wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi
ya wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakimsikiliza Meneja
Mikakati wa TBL Group,Magabe Maasa ,(kulia) wakati wa uzinduzi wa
program hiyo.
Meneja
ukuzaji vipaji wa TBL Group,Lilian Makau ,na Meneja vipaji wa ABInBev
Afrika , Cindy Rautenrouch (kulia) wakiwaonyesha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) jinsi ya kutuma maombi ya kozi ya mafunzo kwa njia ya mtandao wa internet
…………………..
Wasomi
nchini hususani wahitimu wa vyuo vikuu wanaotarajia kumalizia masomo
yao mwaka huu wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na mafunzo ya
kimataifa ya uongozi wa kibiashara ambayo yameanzishwa nchini na kampuni mama ya TBL Group ya ABIn Bev.
Akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mlimani wakati wakati
wa uzinduzi wa program ya mafunzo haya nchini,Meneja wa ukuzaji vipaji
wa ABInBev kanda ya Afrika,Cindy Rautenrouch,amesema kuwa mafunzo haya yameishaonyesha mafanikio makubwa katika nchi ambazo kampuni hiyo inaendesha biashara zake na sasa ndio yamezinduliwa rasmi barani Afrika.
Alisema
katika kipindi cha awamu ya kwanza ya mafunzo haya zimechaguliwa nchi
za Afrika ya Kusini,Tanzania,Kenya na Nigeria na lengo kubwa ni kuwanoa
vijana wahitimu wasio na uzoefu wa kazi kupata elimu na uzoefu na
wakishahitimu kupatiwa fursa za uongozi wa vitengo mbalimbali katika
biashara za kampuni zilizopo kwenye nchi mbalimbali.
“Ndoto
yetu kubwa kama kampuni ni kuwaleta watu pamoja katika ulimwengu
maridhawa (Better World) katika kutimiza ndoto hii na kuhakikisha bidhaa
zetu zinaingia katika masoko mapya moja ya mkakati wake ni kuvutia
wateja wapya na kuondoa mipaka na ndio maana tunatoa fursa kwa wote
kujiunga na kufanya kazi na sisi”.Alisema Rautenrouch.
Alisisitiza
kuwa hii ni fursa pekee kwa wahitimu wa Kitanzania kutoka vyuo vikuu
vyote. wanachopaswa kufanya ni kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao na
wale watakaokidhi vigezo na kuchaguliwa wataungana na wenzao kutoka
mataifa mbalimbali kupatiwa mafunzo kwenye program hii ijulikanayo kama
Global Management Training Programme.
Rautenrouch alisema kwa watakaofanikiwa kujiunga
watapata mafunzo kwa muda wa miezi 10 mfululizo ambapo wanapata mafunzo
ya nadharia na vitendo ndani na nje ya kampuni kwenye nchi mbalimbali
na kukutanishwa na kuzungumza na wataalamu waliobobea katika fani
mbalimbali za uendeshaji wa biashara na utawala.
“Wahitimu
walengwa zaidi katika program hii ni waliohitimu katika fani za
Biashara,Uchumi,Masoko,Uhasibu na fedha,Uhandisi na IT na fani
nyinginezo wenye vipaji kwa kuwa kampuni yetu inaamini katika kuwekeza
katika viongozi wa baadaye na ndio maana tumekuja na mpango wa kuwaandaa”.Alisema.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliohudhuria semina ya uzinduzi,Paul Melkior anayesoma shahada ya kwanza
ya baiashara alipongeza jitihada hizi na kuongeza kusema kuwa uwekezaji
unaolenga kuleta manufaa kwa jamii ndio unaotakiwa kwa kuwa unafungua
milango ya ajira kwa watanzania na kuwapatia fursa za uongozi wazawa baada ya kupatiwa mafunzo ya kitaalamu.
No comments :
Post a Comment