Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB
Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akimkabidhi hundi kifani yenye
thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.032/- Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe.Dkt. Phillip Mpango. Gawio hilo limetolewa kwa Serikali baada ya
benki hiyo kupata faida ya shilingi Bilioni 15 mwaka jana. Wa kwanza
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dorothy
Mwanyika na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB
Sabasaba Moshingi. Tukio hilo ilifanyika kwenye Makao Makuu ya Wizara ya
Fedha na Mipango, Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB
Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akikabidhi hundi kifani yenye
thamani ya shilingi Milioni Tisini na Saba kwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Shirika la Posta Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Kondo kwenye
tukio la kukabidhi gawio kwa wanahisa wa benki hiyo. Akishuhudia ni
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango. Wa pili kulia ni
Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Dodoma Thobias Lawrence na Posta
Masta Mkuu wa Shirika la Posta Deogratius Kwiyukwa.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango, akisisitiza jambo wakati Benki ya Posta (TPB Bank Plc)
ilipokabidhi Serikalini gawio la shilingi bilioni 1.032 kwa mara ya
kwanza Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Puma, Dkt. Ben Moshi (Kulia), akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Philip Mpango, hundi kifani ya shilingi bilioni 7, ikiwa ni gawio
la Kampuni hiyo baada kupata faida kwenye biashara ya kuuza mafuta mwa
ka fedha uliopita. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw.
Philipe Corsaletti, tukio lililofanyika mjini Dodoma
Meneja wa Kampuni ya Kuhifadhi
Mafuta-Tiper, Bw. Emmanuel Kondi, akipeana mkono na Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango baada ya Kampuni yake kutoa gawio la shilingi
bilioni 2 Serikalini, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini
Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tiper Bw. Stephane Gay.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB
Profesa Lettice Rutashobya (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
TPB Sabasaba Moshingi wakipiga makofi wakati Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Philip Mpango, akitoa nasha zake, wakati Benki hiyo
ilipokabidhi hundi kifani yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni
1.032/- ikiwa ni gawio lao kwa Serikali inayomiliki hisa 86.17 katika
Benki hiyo. Tukio hilo ilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na
Mipango, Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Shirika la Posta Tanzania, Dkt. Haruni Kondo akisisitiza jambo wakati
akiishukuru Banki ya TPB kwa kulipatia shirika lake gawio la shilingi
milioni 97.6 baada ya Benki hiyo kupata faida.
…………………………
Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma
SERIKALI imepokea gawio la zaidi
ya shilingi bilioni 10 kutoka taasisi tatu ikiwemo TPB bank, na kampuni
mbili za mafuta za Tiper na Puma ambazo serikali inamiliki hisa zake.
Taasisi ya kwanza kuwasilisha
gawio hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango mjini
Dodoma ni Benki ya TPB ambayo mwenyekiti wake Profesa Lettice Rutashobya
amekabidhi hundi kifani ya shilingi bilioni 1.032, ikifuatiwa na
Kampuni ya ...
kuhihadhi mafuta ya Tiper iliyowasilisha gawio la shilingi
bilioni 2.
Kampuni ya mafuta ya Puma
ikahitimisha zoezi hilo kwa kukabidhi hundi kifani ya shilingi bilioni 7
ambazo ni sehemu ya faida ya shilingi bilioni 14 ambazo kampuni hiyo
imepata baada ya kulipa kodi.
Akizungumza katika tukio hilo
lililofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma,
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amezipongeza taasisi hizo
na amezitaka Taasisi za Serikali na mashirika ya umma kuilipa Serikali
gawio la hisa zake na zijiendeshe kwa ufanisi na kwa faida ili makusanyo
hayo yaweze kuwahudumia wananchi.
Dkt. Mpango amerejea kauli yake
aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti Kuu kwamba
Serikali itatoa kipaumbele kwa kufanya biashara na taasisi zake za Umma
ili ziweze kujiimarisha kimapato na hatimaye kutoa gawio Serikalini.
“Leo ni siku nzuri sana kwa
watanzania kwa sababu Serikali inapokea gawio la shilingi bilioni 10 kwa
niaba yao lakini fedha hizi hazitoshi nataka mfanye vizuri zaidi ili
gawio liweze kuongezeka ili tuzielekeze kutatua kero zinazoikabili jamii
ikiwemo elimu, afya na maji” alilisisitiza Dkt. Mpango.
Katika tukio hilo pia, Benki ya
TPB Plc imelipatia Shirika la Posta kiasi cha shilingi milioni 97.8
ikiwa ni gawio kulingana na hisa zake asilimia 7.98 inazomiliki katika
Benki hiyo.
Akipokea hundi kifani ya kiasi
hicho cha gawio, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta
nchini, Dkt. Haruni Ramadhan Kondo, ameiomba Serikali ililipe shirika
lake kiasi cha shilingi bilioni 3.6 ambazo ni malipo ya pensheni ya
wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambapo Shirika limelipa pensheni hizo kwa niaba ya Serikali
ili liweze kuongeza mtaji na kujiendesha kwa faida zaidi.
Awali Wenyeviti wa Bodi za
wakurugenzi wa Taasisi hizo wameahidi kuendelea kufanya biashara kwa
umahili mkubwa ili kuongeza gawio kwa wanahisa wake na kuiomba iwawekee
mazingira yatakayosaidia kufanikisha azma yao hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya TPB Bank, Profesa Lettice Rutashobya, amesema kuwa Benki yake
imeendelea kukua kwa kasi, kuimarika na kufanya vizuri katika biashara
ya fedha pamoja na kuwa mahili katika ubunifu na kuwa tishio kwa taasisi
nyingine za fedha.
Nae Meneja wa Kampuni ya Kuhifadhi
Mafuta-Tiper, Bw. Emmanuel Kondi, ameiomba Serikali kuiwezesha kampuni
hiyo kufanya biashara kwa mafanikio zaidi hivyo kuongeza gawio ikiwemo
kuangalia upya mfumo wa himaya moja ya Forodha ambao amesema pamoja na
kuwa na ufanisi mkubwa una baadhi ya changamoto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Kuuza Mafuta-Puma, Dkt. Ben Moshi amesema
kuwa Kampuni yake ilitengeneza faida na kuiwezesha kutoa gawio la
shilingi bilioni 7 kwa Serikali ikilinganishwa na shilingi bilioni 4.5
ilizotoa mwaka wa fedha uliopita.
Utaratibu wa Taasisi za
Serikali na mashirika ya umma kulipa gawio la hisa kwa Serikali na
wanahisa wengine ni maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuhakikisha kuwa Taasisi hizo
zinafanya kazi kwa ufanisi, kuzalisha faida na kutoa gawio kwa Serikali
ili mapato hayo yaweze kuhudumia wananchi katika Nyanja mbali mbali
kama vile huduma za afya, elimu, maji na barabara.
No comments :
Post a Comment