Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Charles Mwijage akiwatambulisha Mstahiki Meya wa Jiji la Dar
es Salaam Mhe. Issaya Mwita (kulia) na Meya wa Manispaa ya Kinondoni
Mhe. Benjamin Sitta kwa ugeni kutoka Oman walipotembelea katika Maonesho
ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Kinondoni Benjamin Sitta akisalimiana na Meneja Masoko na Mawasiliano wa
Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), Bw. James Mlowe
alipotombelea banda la Mfuko huo wakati wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa
ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo. Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji
la Dar es Salaam Mhe. Issaya Mwita.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe. Issaya Mwita akimwelezea jambo Mkurugenzi Mkuu wa SIDO
Tanzania Mhandisi. Profesa Sylivester Mpanduji alipotembelea banda lao
katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.
Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe. Issaya Mwita na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh.
Benjamin Sitta wakitazama ramani ya miradi ya makazi inayojengwa katika
eneo la Kigamboni na Kampuni ya Internatinal Property walipotembelea
banda la Kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es
Salaam (DITF) leo. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Saleh
Omar Saleh.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe. Issaya Mwita na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh.
Benjamin Sitta wakipata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) walipotembelea banda la Kampuni hiyo
katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam akipata huduma ya kupima urefu mara baada ya kupima presha
alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika
Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe. Issaya Mwita(kulia) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Kinondoni Mh. Benjamin Sitta (kulia kwake) wakisikiliza namna mfumo wa
Automotive unavyofanyakazi banda la VETA katika Maonesho ya Kimataifa
ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa
VETA Bw. Peter Sitta.
Na: Frank Shija – MAELEZO
…………………………..
Na: Frank Shija -MAELEZO
Halmashauri nchini zimetakiwa
kutumia vyema fedha zinazotengwa kwa ajili ya kundi la vijana na
wanawake katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kuifanya
Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa Kati na Viwanda.
Hayo yamebainishwa leo na Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam alipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa
ya Biashara Dar es Salaam (DITF) mabapo katika ziara hiyo aliambatana
na Mstahiuki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Benjamin Sitta.
“Taasisi za kifedha zinao wajibu
mkubwa katika kufikia adhima hii ya Serikali, lakini sisi Serikali za
mitaa, Halmashauri ziano wajibu mkubwa kuhakikisha zilie asilimia tano
za vijana na tano za wanawake zinakuwa sehemu ya kuchochea ufanikishaji
wa dhamira njema ya Serikali,” alisema Mhe. Mwita.
Aidha Mhe. Mwita ametoa pongezi
kwa uongozi wa Tantrade kutokana na jitihada zao za kuhakikisha
wanasaidia ukuaji wa bidhaa za ndani hasa bidhaa za ngozi ambapo
alisisitiza ni vyema wakaendelea kuweka mkazo katika eneo hilo kabla ya
kuangalia maeneo mengine.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa
ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta amesema kuwa Maonesho hayo ya Sabababa
yamekuwa na manufaa kwa wafanyabiashara wengi na hata kwa wananchi kuja
kujifunza.
Aliongeza kuwa pamoja na wananchi
kuja kujifunza lakini pia imekuwa ni fursa kwa wafanyabiashara
kutengeneza mahusiano na wafanyabiashara wenzao kutoka nchi nyingine
jambo ambalo katika biashara ni muhimu sana.
Nae, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin Ratageruka amesema
kuwa dhamira yake ni kuhakikisha bidhaa za ndani zinakuwa na soko la
uhakika ndani na nchi ya nchi.
Ameongeza kuwa kwa kuanzia
wamejikita zaidi katika bidhaa za ngozi ikiwa ni njia pia ya kuwainua
wafugaji ambao mazao ya mifugo yao yanatumika katika kutengeneza bidhaa
mbalimbali za ngozi.
“Serikali inatambua umuhimu wa
kuthamini bidhaa za ndani, ndiyo sababu Ofisi ya Waziri Mkuu iliratibu
zoezi ambalo jumla ya vijana 1000 walipatiwa mafunzo ya usindikaji na
ushonaji wa ngozi, katika mafunzo yaliyofanyika Chuo cha Teknolojia Dar
es Salaam tawi la Mwanza,” alisema Rutageruka.
Rutageruka ameongeza kuwa katika
kuendeleza jitihada hizo Gereza la Karanga (Moshi) na Kampuni ya Woisso
ya Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuanzisha viwanda kwa ajili ya
kutengeneza sole ili kuachana na utaratibu wa kuagiza skutoka nje.
Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya
Biashara Dar es Salaam yanafanyika huku azma ya Serikali ya Awamu ya
Tano ikiwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati na
viwanda, kutokana na dhamira hiyo maonesho haya yamepewa kauli mibu
isemayo; “Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda.”
No comments :
Post a Comment