Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa
awamu ya Tatu, Mhe.Benjamin William Mkapa, wilayani Chato mkoani Geita leo
Julai 9, 2017. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho Julai 10 anatarajiwa
kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya
(Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita.(PICAH NA IKULU)
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa
Japan hapa nchini Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita.
Balozi huyo wa Japan katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa
kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa
Msaada wa Serikali ya Japan.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais
mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais mstaafu wa awamu
ya Tatu Benjamin William Mkapa pamoja na wageni mbalimbali waliofika Chato kwa
ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita
Josheph Kasheku Msukuma aliyefika Chato pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita





No comments :
Post a Comment