Wakati
wa sherehe, wanafunzi waliofanya vizuri walizawadiwa na kupongezwa na
mgeni rasmi ambapo waliopongezwa ni walinzi wawili ambao waliweza kuzuia
wezi wa mali za wateja wao wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao.
OCD
Simba alikuwa mgeni rasmi katika gwaride la kufuzu mafunzo ya maofisa
75 ambao wamekamilisha mafunzo ya msingi ya ulinzi katika sherehe
zilizofanyika siku ya jumamosi tarehe 29, Julai 2017 katika kituo cha
mafunzo cha SGA kilichopo Mbezi Beach.
Maofisa
75 tu ndio waliofuzu mafunzo kati ya 179 ambao walikuwa wanapatiwa
mafunzo, jambo linaloonyesha viwango vya juu vya mafunzo ambapo
waliobakia wataendelea na mafunzo.
Vilevile
OCD Simba alikagua vifaa ya kampuni ikiwemo magari ya dharura, magari
ya zima moto na chumba cha mfumo wa kuongoza mawasiliano. Alifurahishwa
na uwekezaji uliowekwa na kampuni hiyo na udhibiti ambao uko katika
utendaji kazi wao, hasa mfumo wa kufuatilia.
Maneja
Rasilimali watu wa (HRM) Ebenezer Kaale, alieleza kuwa mafunzo hayo
yalikuwa yanajumuisha vitengo vingi wakiwemo huduma kwa wateja, zima
moto, huduma ya kwanza, misingi ya haki za binadamu miongoni mwa vitengo
vingi vya muhimu vya kiulinzi.
“Tunaamini kwamba tumewapatia mafunzo ya msingi ya ulinzi kuweza kuwawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi”, alisema.
Kabla
ya kuajiri, mchujo na uchunguzi wa kina wa maombi yote. Alama za
vidole huchukuliwa kwaajili ya kukagua taarifa za makosa kwa maofisa wa
Wizara ya Mambo ya Ndani huku uchunguzi wa kidaktari hufanyika kwaajili
ya kukagua uwezo na stamina kabla ya kuanza mafunzo.
Ni
utamadumi wa kampuni hii ya ulinzi kutambua utendaji wa kiwango cha
juu, vyeti na fedha taslimu viliyolewa wakati wa gwaride kuwahamasisha
wengine.
Vilevile
alikuwepo RCO SSP wa Kinondoni John Malulu, ambaye alikuwa OCD wa Kawe.
Mr Malulu aliipongeza kampuni ya ulinzi ya SGA kwa ushirikaiano
iliyokuwa ikitoa wakati akiwa kiongozi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kawe,
kwa kusema kwamba ushirikiano wao ulifanya kazi ya upolisi kuwa nyepesi.
Alibainisha
kwamba SGA ilitoa magari kwaajili ya doria siku za mwisho wa wiki na
siku za sikukuu na kusaidia polisi katika kufanya ukarabati baadhi ya
magari yake.
“SGA
ilikuwa ya kwanza kuitika wateja wao na majirani zake na hiyo ilisaidia
kupunguza kiwango cha uhalifu. Ninatarajia msaada na ushirikiano wenu
katika nafasi yangu mpya.” Aliongeza.
Mkurugenzi
wa kampuni ya ulinzi ya SGA bwana Eric Sambu, amesema kwamba kampuni
hii ni kubwa kuliko zote hapa Tanzania, na inatilia mkazo katika mafunzo
kuwapa uwezo wafanyakazi wao kuweza kutekeleza majukumu yao, ili kuweza
kufikia na kuzidi matarajio ya wateja wao.
“mafunzo kwetu mi kiungo muhimu katika mafanikio yetu na tunatilia mkazo kila aina ya wafanyakazi nchini.”, aliongeza.
Walihitimisha
jana mafunzo mengine kwaajili ya timu ya ukaguzi wa fedha ya ndani
kwajili ya ISO 9001: 2015, kuhusu Udhibiti wa Ubora, ambayo kampuni hii
ithibitishwa tangu 2001.
Kampuni
ya ulinzi ya SGA inatoa huduma ya ulinzi, kusafirisha fedha, ulinzi kwa
njia ya mitambo ya kielektroniki, huduma ya muito kwa alarm, huduma ya
kufuatilia vyombo vya moto, usafirishaji wa mizigo pamoja na kazi zingine.
Inaendesha pia shughuli zake nchi nzima na ina wafanyakazi wapatao 5,000 na wateja kutoka katika kila sekta ya uchumi.
![]() |
| Baadhi ya viongozi wakisikiliza |
![]() |
| Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi Joakim Sabana akizungumza kwenye hafla hiyo. |
![]() |
| Baadhi ya viongozi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, wakiimba wimbo wa Taifa |
![]() |
| Baadhi ya viongozi wakitambulishwa. |
![]() |
| Askari wa kampuni hiyo wakijiweka tayari kabla ya ukaguzi wa gwaride. |




















No comments :
Post a Comment